MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI SEPT 27
Mtihani
kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa
na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Septemba
27 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF).
Kwa
wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni
mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani
huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni maswali kutoka FIFA
wakati nyingine ni kutoka TFF. Ada ya mtihani ni dola 50 za Marekani.
No comments:
Post a Comment