Thursday, August 30, 2012

ASEMAVYO MWAKYEMBE - ARUSHA


Hali ninayoiona sasa katika Taifa letu ni kuwa watu waliokuwa na uwezo wa kulisaidia Taifa kwa maombi na kuugua kwa ajili ya Nchi, wameanza kupotelea katika mifumo ya kisiasa, watu waliokuwa na mzigo wa kufunga na kulia kila siku mbele za Mungu kwa ajili ya nchi, sasa wameanza kupungua sana, na waliobaki wanaanza kujaribu kupigana mwilini moja kwa moja na kusahau asili ya Tatizo, yaani tumeanza kupambana na mashina na kusahau mizizi, tukumbuke neno linasema “Enyi wenye kumkumbusha Mungu msiwe na kimya wala msimwache yeye akae kimya mpaka atakapofanya imara kuta za yerusalemu … maana yake ni tuendelee kuomba na kuomba mpaka atakapotenda. na nivizuri tukaelewa kuwa kila aliyempokea kristo ni wajibu wake kumkumbusha Mungu kwa maombi na sara kwa kulia na toba kila siku kwa habari ya nini tunataka kitokee juu ya Taifa

letu. Lengo langu ni hili tuelewe kuwa pamoja na mambo mengine yote tunayohusika nayo kisiasa, misimamo tuliyonayo kisiasa bado Mungu muumba wa mbingu na nchi ndie mwenye majibu ya nini hasa watanzania tunahitaji kwa sasa, hivyo basi ninakutia moyo kuendelea mbele na harakati za kutaka kuona mabadiliko juu ya nchi lakini ukiizingatia mistari ifuatayo Yoh 15:5b “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote…” Haya ni maneno ya Bwana Yesu kwa kanisa akionyesha kuwa tunaitaji msaada wa Mungu kwa asilimia mia moja kwa kila jambo tunalolihitaji.

Lakini pia Mtume Paulo anasema “kushindana kwetu sisi si juu ya Damu na nyama; Bali ni juu ya falme na mamlaka,juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa Roho” hii ni Efeso 6:12. Sasa basi tuelewe kuwa huku rohoni ndiko kwenye chanzo cha kila tatizo ndiko kwenye mizizi ndiko kwenye mifumo ndiko huwa kunaitwa jikoni, hivyo tuanze kujifunza kuanzia jikoni kwenda sebuleni na si kuanzia sebuleni alafu tukikosa tunachokitaka mezani ndipo twende jikoni, tutakuwa tumechelewa sana. Kumbuka Fil 4:6 nini anasema “Msijisumbue kwa neno lolote bali katika kila neno kwa kuomba …. Haja zenu na zijulikane na Mungu …”, anaposema msijisumbue kwa neno lolote hana maana tusifanye hapana, isipokuwa tupoamua kufanya jambo lolote tukumbuke kuwa Mungu atatakiwa kuhuhusika kwa asilimia mia moja , faida zake ni kuwa atakupa ulinzi, atakupa hekima na atakuwa akikuongoza nini cha kufanya, nini kusudi lake, na hivyo utafanikiwa chini ya mkono wa Mungu …

Itaendelea
Mkaribishe na mwingine kusoma ujumbe huu 
Tuntufye Mwakyembe wa CHANGING YOUTH CHANGING NATION-ARUSHA

1 comment: