POLISI WASEMA ALIYEKUFA KWENYE MAANDAMANO MORO HAKUPIGWA RISASI
Sarah Mgaji, Morogoro Yetu
Jeshi
la Polisi Mkoani Morogoro limesema kuwa marehemu Ally Singano
aliyeuawa wakati wa vurugu zailizotokea mkoani humo juzi hakupigwa
risasi bali alikufa kutokana na kurushiwa kitu chenya ncha kali
kilichosababishamajeraha na kupoteza maisha.
Ally
Singano aliuawa katika vurugu zilizotokea baada ya Polisi kuzuia
maandamano yaliyokuwa yakifanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema ) mjini Morogoro.
Akitoa taarifa ya
uchunguzi wa mwili wa marehemu uliofanyika chini ya madaktari wawili
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Faustine Shilogile amesema kuwa uchunguzi
uliofanyika umebaini kuwa marehemu Ally Singano alikuwa na majeraha
kichwani ambayo yalisababishwa na kurushiwa kitu kilichomgonga kichwani
na kumsababishia majeraha hayo makubwa hadi kufikwa na mauti.
Kamanda
Shilogile amesema taarifa za kutumika risasi za moto na kusababisha
kifo cha kijana huyo sio sahihi na kwamba ni mabomu ya machozi ndiyo
yaliyotumika kutawanya maandamano hayo.
Aidha
kamanda Shilogile amesema uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini ni
kitu gani kilichotumika kumpiga mtu huyo na nani aliyehusika na kumpiga
ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani wale wote walioandaa
maandamano hayo.
Hata hivyo hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa
kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana hao.
Jana
jioni Polisi walisafirisha miwili wa marehemu kwenda mkoani Tanga
ambako ndiyo mazishi yatafanyika.
No comments:
Post a Comment