Friday, September 28, 2012

Je zito Kabwe ataweza kuvaa kiatu cha Dr. slaa 2015?

zito kabwe akihutubia moja ya mikutano ya chama.
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe amesema hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015 badala yake anajipanga kuwania urais.
 Zitto alisema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliokuwa unafanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma.Zaidi ya watu 200, ambao walihudhuria katika mjadala huo wa wazi walimuuliza maswali mbalimbali mbunge huyo, huku mmoja akigusia kuhusu tetesi za mara kwamba Zitto anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.“Nimefanya kazi kubwa katika kazi yangu ya ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni  mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka kumi.
 “Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola,” alisema Zitto.“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.
 “Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.
 Katika hatua nyingine Zitto alisema ana mpango wa kuwania urais kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
 “Kwanza nataka niwahakikishia watu wa Kigoma msiwe wanyonge…mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii,” Zitto alianza kujibu swali hilo na kuendelea.
 Hata hivyo Zitto alipoulizwa baadaye  kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa katiba alijibu; “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndio maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika katiba mpya.”
 “Nchi za Kidemokrasia lazima vyama vibadilishane utawala wa kuongoza nchi  kama ilivyo katika nchi za Ghana na Zambia. Tanzania inatakiwa kuiga mfano wa nchi hizo,” alisema Zitto
 Katika kukazia hilo, Zitto alisema anashangazwa na umaskini uliopo Tanzania wakati mwaka 1976 uchumi wake ulikuwa sawa na nchi ya Malaysia, lakini mpaka kufikia mwaka 2001, Malaysia ilipunguza idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kutoka asilimia 56 mpaka kufikia asilimia tatu huku Tanzania ikipunguza kutoka  51 mpaka 46.
 Katika hatua nyingine, Zitto alikana kuwa, Chadema ni chama cha udini, ukanda, ukabila  ila akasisitiza kuwa ni chama cha kitaifa.
 “Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu,” alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.
 “CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?” Alihoji Zitto.
 Alisema ili kuthibitisha kuwa Chadema si chama cha Kikanda, matokeo ya urais wa mwaka 2010, Dk Wilbroad Slaa aliongoza dhidi ya wagombea urais wengine kwa kupata kura nyingi katika Jimbo la Manyovu mkoani Kigoma na hivyo kufanya kupata asilimia nyingi kuliko sehemu yoyote Tanzania.

Dk. Willibroad Slaa,jJK NDO ANAIZIKA CCM KWA KUPITISHA WATUHUMIWA WA UFISADI KUGOMBEA NEC.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa, amemvaa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akisema amekitengenezea kaburi la kukizika rasmi chama chake kwa kuruhusu watuhumiwa wakubwa wa ufisadi kugombea nyadhifa mablimbali.
Dk. Slaa alisema uteuzi wa wagombea ndani ya CCM uliomalizika juzi umeonyesha wazi kwamba sasa chama hicho kinatumbukia kwenye dimbwi kubwa na pana lisiloweza kukitoa tena.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Mwanza, alikojichimbia kuhakikisha mchakato wa uchaguzi wa mameya wa jiji hilo unakwenda vizuri leo, Dk. Slaa alisema dhamira ya kweli dhidi ya CCM katika kuwaweka vijana kwenye uongozi ili kukinusuru chama hicho imezimika baada ya Kikwete kuruhusu watuhumiwa wa ufisadi na wakongwe kugombea uongozi.
“Katika hili la uteuzi wa CCM, nangojea taratibu zao zikamilike. Tulitegemea CCM muda huu ni wa kujisafisha, lakini imeshindwa kufanya hivyo. Mimi simung’unyi maneno kuhusu watuhumiwa wa ufisadi.
Mfano (anataja) ni fisadi wa fedha za rada. Mimi hapa nilishapeleka ushahidi hadi wa akaunti namba ya benki yake kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini), alisema.
Alisema inashangaza kuona katika utetezi wa CCM, mtuhumiwa huyo amepatiwa nafasi licha ya kushindwa kueleza wazi fedha nyingi kwenye akaunti hiyo ya Uswisi alizipataje.
“Mtuhumiwa mkubwa kama huyu wa ufisadi eti leo CCM inampitisha awe mgombea. Kweli? Sioni dhamira ya CCM kupambana na vitendo vya kifisadi. Na hata dhamira ya vijana haipo bali imejitumbukiza kwenye dimbwi ambalo kamwe hakitatoka humo,” alisisitiza.
Kuhusu Lowassa na tuhuma zake za ufisadi wa kampuni ya kufua umeme wa dharura wa Richmond zilizosababisha kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, Dk. Slaa alisema kiongozi huyo alilazimika kujiuzulu kama sehemu ya kuwajibika, lakini ameshindwa hadi leo kumtaja mhusika hasa wa kampuni hiyo.
Alisema kama kweli Lowassa alisingiziwa katika tuhuma hizo, alipaswa kuwaeleza Watanzania nani anayehusika na ufisadi huo wa Richmond ambayo ilishindwa kuzalisha umeme licha ya kutumia mamilioni ya fedha za umma.
Kuhusu wanachama wa CCM ambao majina yao yamekatwa na NEC, Dk. Slaa alisema milango iko wazi CHADEMA kwa wale wasio mafisadi kujiunga ili kukielekeza chama hicho kushika dola mwaka 2015.
Alisema CHADEMA ni chama makini huenda kuliko vyama vingine, hivyo hakiwezi kupokea wanachama kutoka CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi, vinginevyo kitafunga milango na mapazia yake.
“Unajua, kuna watu wanaojulikana kwa ufisadi. Pia wapo wasafi wanaoomba kujiunga na CHADEMA, hivyo watu safi hawana tatizo kujiunga na CHADEMA kwa ajili ya kuunganisha nguvu kwenda kuongoza dola mwaka 2015,” alisema Dk. Slaa.

NI CHADEMA VS CCM KATIKA UMEYA JIJINI MWANZA LEO

uchaguzi wa mameya wa wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela jijini Mwanza, unatarajiwa kufanyika leo huku mnyukano mkali ukiwa katika halmashauri ya Nyamagana kutokana na CCM na CHADEMA kuwa na idadi sawa ya viti vya madiwani na hivyo kutegemea kura za CUF ziamue mshindi.
Katika Halmashauri ya Ilemela, CHADEMA ina uhakika wa asilimia mia moja kutokana na kuwa na madiwani wengi kuzidi wenzao wa CCM huku mikakati yao ikilenga kuwashirikisha CUF ili waitwae pia Nyamagana.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kugawanywa na hivyo kuzaa halmashauri hizo mbili. Lakini pia Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa sasa muda kadhaa haikuwa na Meya baada ya Baraza la Madiwani kumvua wadhifa huo, Jackson Manyerere (CHADEMA).
Baada ya meya kuenguliwa, kulizuka mtafaruku ndani ya CHADEMA jijini hapa ambao ulisababisha madiwani wawili kutimuliwa uanachama kwa kile kilichodaiwa ni usaliti wa kuanzisha hoja ya kumtosa kiongozi huyo.
Hivyo kutokana na CHADEMA kutokuwa na madiwani hao, inaingia kwenye uchaguzi wa leo ikiwa na madiwani sita na mbunge Ezekiel Wenje katika wilaya ya Nyamagana wakati wenzao CCM wana madiwani saba na CUF wawili.
Kwa mnyukano huo ni dhahiri kuwa CHADEMA na CCM watakuwa wamefungana kwa kura na hivyo kuhitaji huruma ya madiwani wa CUF ili upande mmoja uibuke kidedea.
Taarifa za uhakika kutoka jijini hapa ni kwamba CHADEMA wamefanya mazungumzo ya kushirikiana na CUF kwa kuwaachia nafasi ya Naibu Meya ambayo itagombewa na diwani wao wa kata ya Mirongo, Daud Mukama.
Kwa halmashauri ya Ilemela CHADEMA wana uhakika wa kuibuka kidedea kutokana na kuwa na madiwani wanane na mbunge Highness Kiwia huku wenzao wa CCM wakiwa na madiwani sita na CUF ina mbunge wa Viti Maalum, Mkiwa Kimwanga.
Kamati za utendaji za CHADEMA katika wilaya hizo zimefanya vikao tofauti kwa kushirikiana na kamati za madiwani na kukamilisha mchakato wa kupata wagombea wao.
Kwa mujibu wa ofisa habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, kamati ya utendaji ya wilaya pamoja na madiwani wa Nyamagana walimteua aliyekuwa Naibu Meya kabla, Diwani wa Kata ya Maina, Charles Chibara, kuwa mgombea wa umeya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Kwa upande wa Ilemela, kikao cha kamati ya utendaji pamoja na madiwani walimteua Diwani wa Kata ya Nyamanoro, Abubakar Kapera, kuwa mgombea wa umeya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Kikao hicho cha Ilemela, pia kilimteua Diwani wa Kirumba, Danny Kahungu, kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Meya halmashauri hiyo wakati kamati ya utendaji ya Nyamagana imekubali kumwachia kugombea nafasi ya Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Diwani wa Mirongo, Daudi Mkama (CUF).
Wao CCM wamemteua Diwani ya Kata ya Mkolani, Stanslaus Mabula, kugombea nafasi ya umeya katika halmashauri ya jiji la Mwanza huku diwani wa kata ya Igogo, John Minja, akigombea unaibu meya na Ilemela wagombea ni Renatus Kalunga na naibu wake Sarah Ng’hwanu.

John Terry aadhibiwa na FA,je unajua kwa nini mahakama ya kiraia ilimkuta hana hatia ?fuatana nasi hapa kwa habari hii kwa kina

John Terry
John Terry amepigwa marufuku ya mechi nne na kutozwa faini ya pauni 220,000
John Terry ameadhibiwa na chama cha kandanda cha England, FA, asicheze mechi nne, na vile vile alipe faini ya pauni 220,000, kutokana na matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand. Chama cha FA kilithibitisha Terry alifanya makosa hayo, baada ya kusikiliza kesi dhidi yake kwa kipindi cha siku nne. Msemaji wa John Terry alisema mchezaji huyo "alisikitishwa" na hatua ya FA, kwa kuamua tofauti, kinyume na mahakama, ambayo awali ilisema hana makosa. 
Mwezi Julai, mahakama ya Westminster mjini London ilipitisha uamuzi kwamba mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 31, hakufanya kosa hilo, la kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Ferdinand.
 Hata hivyo wengi watajiuliza kwa nini adhabu dhidi ya Terry ni nyepesi mno, ikilinganishwa na ile iliyopitishwa dhdi ya mchezaji wa Liverpool, Luis Suarez mwaka jana. Terry ana muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, mara tu atakapopokea maelezo ya adhabu hiyo kupitia maandishi. Adhabu hiyo haitatekelezwa hadi Terry atakapopata nafasi ya kuamua atafanya nini. 
Taarifa kutoka klabu yake ya Chelsea iliongezea: "Klabu ya Chelsea inafahamu vyema uamuzi uliopitishwa, na inaheshimu uamuzi huo uliotolewa leo na chama cha FA kumhusu John Terry."

Thursday, September 27, 2012

Chaguzi za CCM: Undugunisation au majina kufanana tuu?fuatilia habari hii kwa kina hapa uone jinsi ngudu walivyopitishwa kuendelea kula nnchi.

Salma Rashidi KIKWETE
Mwanaisha Halfani KIKWETE
Mohamed Mrisho KIKWETE
Ridhiwani Jakaya KIKWETE

Vita Rashidi Kawawa
Zainab Rashid Kawawa

Bayoum Awadhi KIGWANGALLA
Hamisi Andrea Kigwangalla

Saumu Mohamed BENDERA
Denis William BENDERA
Stanley J. BENDERA
Saum Mohamed BENDERA

William John MALECELA
Anne Kilango MALECELA

Lulu Abbas MTEMVU
Abbas MTEMVU

Sophia Mnyambi SIMBA
Ulanga Agathon SIMBA

Aisha Omar Kigoda
Abdallah Omari KIGODA

Wakati Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekamilisha kazi ya uteuzi wa wagombea uongozi kwenye nafasi mbalimbali za chama hicho, vita kubwa inaonekana kuwa katika nafasi 10 za ujumbe wa Nec kwani mawaziri sita ni miongoini mwa wanachama 31 wa Bara watakaopamba vikali kupata nafasi hizo.
Hali ni hiyo pia kwa uopande wa Zanzibar kwani katika wanachama 28 wanaowania nafasi 10 za Nec Zanzibar, wapo mawaziri wanne.
Mbali na mawaziri sita nafasi 10 za Tanzania Bara pia  kuna wabunge watatu, mkuu wa wilaya mmoja na vigogo wawili wa Kamati Kuu ya chama hicho.
Kwa upande wa Zanzibar wamo mawaziri wanne akiwamo Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.
Mawaziri watakaochuana Bara ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Dk. David Mathayo David; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge),  William Lukuvi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira; Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,  January Makamba.
Pia wamo Katibu Mkuu wa CCM, Willison Mukama, Mbunge wa Iramba Magharibi na Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM, Mwigulu  Nchemba, wote ni wajumbe wa Kamati Kuu.
Wengine ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Shy-Rose Sadrudin Bhanji; Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM),  Martine Shigela na Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama.
  Wamo pia Otieno Peter Baraka, Twalhata Ally Kakurwa, Godwin Emmanuel Kunambi, Innocent Mahendeki Nsena, Richard Hiza Tambwe, Anna John Magowa, Christopher Thomas Mullemwah, Salehe Mbwana Mhando,  Fadhili Emmanuel Nkurlu, Tumsifu Aaron Mwasamale, William John Malecela, Rashid Mrisho Kakozi, Dk. Luteni Kanali Kesi Athuman Mtambo, Nicholaus Daniel Haule na Nussura Gilbert Nzowa.
Wengine ni Hadija Uledi Faraji,  Dk. Hussain Abdulrehenan Hassan na Mwanamanga Juma Mwaduga, Mbunge wa zamani wa Muleba Kaskazini, Ruth Blasio Msafiri na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson William Msome.
Kwa upande wa visiwani walioteuliwa kuwania nafasi hizo Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi; Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Abdallah Juma Sadallah, na Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee,
  Wengine ni  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kukenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Makame Mnyaa Mbarawa pia humo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Wengine ni Kidawa Hamid Saleh, Abdisalaam Issa Khatib,  Khadija Hassan Aboud, Abdalla Ali Hassan, Mohamed Ahmada Salum, Abdulhakim C. Chasama, Ali Mohamed Ali, Haji Makame Ali, Ibrahim Khamis Fataki, Moza Jaku Hassan, Nassir Ali Juma, Jecha Thabit Kombo, Khamis Mbeto Khamis,  Mohamed Hassan Moyo, Bhaguanji M. Mansuria Moudline C. Castico, Yakoub Khalfan Shaha, Rose Joel Mihambo, Ali Omar Mrisho na Mariam Omar Ali.

CHADEMA WAFANYA MKUTANO WA M4C JIJINI ARUSHA HIYO JANA UKWELI HIKI CHAMA KINA UHAI MKUBWA SANA HAPA MKOANI ARUSHA ...!


Wananchi wa jiji la Arusha wakiwasikiliza viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa umakini , katika viwanja vya Kilombero-karibu na hospitali ya Levolosi-Jijini Arusha.
Wananchi wa jiji la Arusha wakifuatilia sera za viongozi wao wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika viwanja vya Kilombero-karibu na hospitali ya Levolosi-Jijini Arusha.
Wananchi wa jiji la Arusha wakiwasikiliza viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),akiwemo aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema, katika viwanja vya Kilombero-karibu na hospitali ya Levolosi-Jijini Arusha.
Wananchi wa jiji la Arusha wakimsikiliza Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassary katika viwanja vya Kilombero-karibu na hospitali ya Levolosi-Jijini Arusha,akisisitiza kuwa Mwenge wa Uhuru jimboni kwake ni MARUFUKU.
Hili ni gari la aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Mhe:Godbless Lema,akiwa katika viwanja vya Kilombero-karibu na hospitali ya Levolosi-Jijini Arusha,akiwaambia wananchi wake kuwa wasijali kesi yake itamalizika mapema na kurudi kazini upya.

Nimeipenda hii advancement,-Lawsuit: $73,000 Glass Pool Table Not Up to Scratch.

Lawsuit: $73,000 Glass Pool Table Not Up to Scratch

Glass Pool Table

$73,000 only.

The buyer of a futuristic, $73,000 glass pool table claims he's been snookered. In a complaint filed in Orange Country, Calif., superior court, the buyer alleges that the maker, Nottage Design of Australia, neglected to disclose one important fact about the table:
Play on it with anything but specially-coated, custom-made balls, and you scratch the glass.
Brant Martin, a Dallas attorney representing the buyer (identified in the suit only as Desert Beach, an LLC) says his client learned this fact the hard way: He bought a $73,000 custom G-1 glass-top table for home use, played on it with "a standard set of pool balls, the kind that might be found in any pool hall," and discovered to his horror that this left the table "scuffed, scratched, damaged—essentially destroyed."
The suit says shipping materials that accompanied the table included a sealed envelope with an inconspicuous notation saying that the balls shipped by Nottage were specially made for use with the table—but that this amounted to the "hiding" of so material a warning.
The buyer feels an injustice has been done, says Martin. The complaint seeks $219,000 in damages. Nottage, asked for comment by ABC News, did not respond.
Nottage's website describes the table's glass surface as protected by Vitrik, a proprietary coating "which allows the balls to roll silently at a near identical rate to a standard cloth table… It's highly durable, completely non-toxic and is transparent." The site says the custom balls it sells are coated with a special finish "compatible" with Vitrik. "Please only use these balls," it advises.
Martin says this warning was added only after his client ruined his table and complained to the company. Prior to that, his client alleges, Nottage's website left buyers with the impression they could play with standard pool balls.
The suit claims that at the time the buyer researched and negotiated his purchase, Nottage never once mentioned that its tables could only be used with its own specially-coated balls.
Jesse Rothberg, store manager at Blatt Billiards in Greenwich Village in Manhattan, says he is familiar with the G-1 glass table, which he first saw at a trade show in Las Vegas. He's also seen a copy of the lawsuit.
The table, he says, "didn't look very viable" to him. "I shot a couple of balls on it, because it was there for the exhibit. We all had the same reaction: nothing spectacular. I wasn't thrilled with the action or the balls."
Blatt, in business since 1923, sells traditional slate-topped, fabric-covered models. In the pantheon of pricey pool tables, what could $73,000 buy you?
"Something pretty spectacular," says Rothberg—a nice antique. Then again, you could get what's in the store's front window: A one-of-a-kind gothic job in teak. Price: $250,000.
Expensive, true; but you play on it with regular old balls.