Friday, April 22, 2016

UONGO,UZUSHI NA UKWELI KUHUSU SIMU ZA MKONONI-YONA FARES MARO

Umewahi kusikia , kusoma na kutazama uwongo mwingi kuhusu simu za mikononi . lengo la makala hii ni kujibu uwongo huo na kutoa ufafanuzi kidogo kwa baadhi ya mambo muhimu .
Simu za mkononi zina mionzi sana , kwahiyo usiweke sehemu nyeti kama katika mifuko ya suruali au shati . Ukweli ni kwamba simu nzuri lazima ipitie majaribio yanayoitwa SAR (Specific Absorption Rating) . Inapokua dukani ina maana imepitia huko na kuthibitishwa ubora wake .
Pia hakuna uhusiano wa matumizi makubwa ya simu na magonjwa uliothibitishwa kisayansi .
Simu ikiwashwa ndani ya ndege inaweza kuingiliana na mitambo ya kuongozea ndege na ni hatari kwahiyo zimezuiwa .
Unachotakiwa kujua ni kwamba mitambo ya kisasa ya mawasiliano na kuongozea ndege imeboreshwa sana . hata ndege iliyojaa watu wote wanaotumia simu za mikono hawata sababisha madhara yoyote .
Kama simu yako ingekua hatari kihivyo basi ungetakiwa kuiacha chini usipande nayo wakati wa ukaguzi au wakati wa taratibu nyingine . Sababu ya kwanini hutakiwi kutumia simu ni ili kuweza kudhibiti abiria na ili uweze kusikiliza matangazo ya mara kwa mara maana usafiri wa ndege unajulikana changamoto zake .
Simu zinaweza kusababisha moto au milipuko katika vituo vya mafuta .
Petroli na mafuta ya aina nyingine yanaweza kuwashwa kwa cheche tu . Lakini cheche inaweza kutoka katika kiberiti , viwashio au hitilafu za umeme ila sio kutoka kwenye simu yako . Hofu iliyopo ni kwamba simu yeye tatizo au betrii inaweza kusababisha cheche na moto lakini hii ni ngumu na hakuna matukio kama hayo yaliyowahi kuripotiwa .
Hautakiwi kuchaji simu usiku mzima : itafupisha maisha ya betrii na kuharibu kifaa chako . Mimi huwa nachaji simu usiku wakati wa kulala lakini huwa nazima .
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba , vifa vyote vya kisasa vyenye betrii huwa na soketi ndani inayozuia isijichaji zaidi kwahiyo kuzuia uharibifu wowote . Betri ikishajaa , itaacha kujichaji yenyewe . Lakini kifaa kinaweza kuendelea kupeleka moto kutokana na sababu kadhaa haswa kama simu imewashwa ikiwa labda inapigwa sana au inafanya shuguli nyingine .
Hapo rejea kwenye suala la kununua vifaa orijino maana vitaweza kukuepusha na matatizo kama hayo .
Ukubwa wa Betrii maana yake betrii itakayodumu zaidi .
Iwe laptop , simu ya mkono au kifaa chochote kinachotumia betrii , uhai wa betrii unahusiana na jinsi kifaa kinavyotumika haswa kwenye suala la umeme .
Unaponunua kifaa chako kikiwa kipya soma makaratasi ya maelezo au ingia katika mtandao utasoma mengi kuhusu utunzaji wa kifaa chako na utadumu nacho kwa muda mrefu .
Utumiaji wa Intaneti kutumia simu ya mkono ni salama zaidi kutoka kwa wahalifu na watu wengine wanaokufuatilia .
Kila simu ina Kivinjari ( Browser ) yenye kitu kinachoitwa incognito mode yenye kuweza kukufanya uwe kibinafsi zaidi lakini hii inazuia kuacha historia isijihifadhi katika kifaa chako . Haitaweza kuficha majina yako , ulipo sasa hivi , shuguli unazofanya , tovuti au blogu ulizotembea , haiwezi kukuficha kutoka kwa polisi au wamiliki wa huduma ya mawasiliano unayotumia kama ni VODA , AIRTEL , TIGO , TTCL .
Usipige simu wakati simu yako iko kwenye chaji kwa sababu inaweza kulipuka .
Ni kweli kwamba kumewahi kutokea matukio kadhaa ya simu na vifaa vingine kulipuka , lakini ni betri za vifaa husika ndizo zinazosababisha moto na kulipuka sio kifaa chenyewe .
Kwababu simu au betri inaweza kuwa feki na yenye kiwango kidogo cha ubora , au ni zile zilizotumika na kuuzwa tena . Kama ukitumia betrii na chaji original kwa jinsi unavyotakiwa kutumia hautapata matatizo kama hayo hata kidogo .
Kwa suala hili , tujihadhari na simu za mikononi tusizojua ubora wala zilikotoka maana matatizo huanzia hapo .
Kwa kuwa TCRA imetangaza kufungia simu feki baadaye mwaka huu , naamini kutakua na simu za maana mitaani na matatizo kama haya yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa kama sio kuisha kabisa baada ya muda mfupi .
Nakutakia matumizi salama ya kifaa chako cha mawasiliano kwa ajili ya kuzalisha , kujenga uchumi , upendo , amani na mshikamano lakini sio kinyume chake .
Mwisho napenda kusema kwamba sifanyi kampuni yoyote ya simu wala sihusiki na biashara yoyote inayohusu simu kwahiyo sina maslahi yoyote katika somo hili zaidi ya kuona wenzangu wanaelimika na kuondoa hofu .
YONA FARES MARO
0786 806028

No comments:

Post a Comment