( Kwa Egon Sakina )
Youth Night live ni maalum kwa vijana kwaajili ya kuwamsha kiuwezo na akili zao pia kuwafanya waweze kuamka kiroho ili wawe chachu ya maendeleo ya kanisa na taifa kwa ujumla.Imekuwa kwa vijana kwa sababu vijana ndio nguzo ya taifa na kanisa, vijana watarajie kubadilika na pia kukutana na Mungu, kutakuwa na maombezi maalum ya vijana katika sehemu mbalimbali za maisha yao na kuombea taifa kwa ujumla.Watakuwepo viongoozi wa serikali na wa kanisa pia maaskofu na wachungaji watakuwepo.
Walimu nao watakuwepo akiwemo Shemeji Melelayeki, Emmanuel Mkwaya, Fred Chavala na Filex Ntambara toka Uganda.
Vikundi vitakavyo hudumu katika usiku huu wa vijana watakuwepo Shangwe Voices, PCASF Praise Team, Rhema Worship Team, New Life Band na Abednego &The Worshipperz intl.
Tukio hili litarushwa live online radio ya Arusha Mambo FM unaweza kupakuwa(Download) Tunein kisha tafuta Arusha mambo.Kijana usipange kukosa usiku huu.
Pia blogger wengi tutakwepo kukuhabarisha live toka eneo la Tukio.
No comments:
Post a Comment