Thursday, September 5, 2013

ndugu wanavujno na viunga vyake

Ndugu wana VUNJO!


Natangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge wa jimbo la VUNJO 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),

huu ni uamuzi wangu binafsi na wa kidemokrasia kwa kuzingatia misingi ya sheria na katiba ya nchi pamoja na ya chama changu,

ninaamini ninazo hoja za msingi, uwezo na kipaji cha kipekee katika kutimiza azma yangu ya kuwatumikia wana Kilimanjaro na Taifa kwa ujumla.

Ninaamini ya kuwa, yapo mambo ya msingi sana ambayo yanahitaji uwepo wangu wa moja kwa moja katika kuyafanya na kuyasimamia mwenyewe kwani mtu mwingine hawezi kufanya kwa weledi kama nilivyokusudia mimi.

Natambua mengi mema aliyoyafaya na anayoyafanya Mhe MREMA, lakini pia ikumbukwe uwezo wetu wa kufikiri ni tofauti, anayoyafikiri Mhe MREMA AU MWINGINE YOYOTE inaweza isiwe ndivyo ninayofikiri mimi,

*NATAMANI KUONA MATUMAINI MAPYA KATIKA VUNJO NA TAIFA LANGU,

*NATAMANI KUONA FIKRA MPYA NA ZENYE UHAI KATIKA NCHI,

*NATAMANI KIZAZI CHENYE MITAZAMO CHANYA KWA KUMAANISHA,

*NATAMANI KUONA MATOKEO MAPYA NA MATUNDA MEMA KATIKA VIWANGO VYA JUU ZAIDI KWA MAENDELEO YA VUNJO NA TAIFA ZIMA,

NB: CHANGAMOTO HAI NA ZENYE MANUFAA HULETWA NA KIZAZI KINACHOFIKIRI SAWASAWA, mimi ni mmoja wapo.

Natambua ugumu uliopo katika safari hii hasa ikizingatiwa kuwa MheMREMA ana wafuasi wengi, jambo hili ninanipa fursa nzuri ya kujiandaa vyema kama ilivyosemwa "BELIEF CREATES THE ACTUAL FACT" ALBERT EINSTEIN.

wenu
MWANAVUNJO MTIIFU NA JASIRI

Wednesday, September 4, 2013

Arsenal wamevunja rekodi yao KATIKA USAJILI WA OZIL

Arsenal wamevunja rekodi yao kwa kumnasa Mmoja ya wachezaji bora Barani Ulaya, Mesut Ozil kutoka Real Madrid kwa pauni milioni 42.4 saa chache kabla dirisha la usajili kufungwa. 


Kiungo Mshambuliaji huyo kutoka ujerumani amepewa mkataba wa Miaka 5 na amemaliza kiu ya mashabiki wa Arsenal waliotaka mchezaji mwenye uwezo na jina kubwa kuletwa kwenye timu yao. Usajili wa Ozil umegharimu zaidi kuliko usajili wa mchezaji Dennis Bergkamp.

Ozili anategemewa kuongeza kasi ya ushambuliajina na kutengeneza mazingira mazuri ya Arsenal Kushinda Premier League.

Tottenham ndio klabu iliyotumia zaidi kwenye dirisha hili la usajili kwakutumia pauni milioni 105 kusajili wachezaji saba na kumpoteza Gareth Bale kwa Real  kwa pauni milioni 85.3

Shujaa wa Injili Tanzania Hayati Dr. Moses Kulola azikwa na maeflu hii leo huko Mwanza wakiongozwa na MH. JK

Siku ya leo Mchana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete amewaongoza maelfu ya Watanzania kuuzika mwili wa Shujaa wa Injili Tanzania Hayati Dr. Moses Kulola aliyezikwa katika Kanisa la Bugando, Mwanza.

Mhe. Kikwete waliongoza viongozi na waumini wa dini mbalimbali, viongozi wa vyama vya Siasa nchini katika Kutoa salamu za mwisho na kuulaza Mwili wa shujaa huyo aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita. Shujaa wa Injili Dr. Kulola aliyezaliwa mwaka 1930 ameelezewa na Mhe. Rais kama ni mtu aliyejitoa kwa ajili ya kazi ya injili katika Tanzania na Nje ya Tanzania.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana linarikiwe.
Mke wa Shujaa wa Injili akiweka Shada ya Maua

Mhe. Wenje akiweka udongo katika Kaburi
Mhe Rais JK akitoa salamu za Mwisho
Mama Josephine Slaa akiweka udongo
Mhe. Slaa akiweka Udongo kwenye Kaburi
Mhe. Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akiweka Shada la maua
Mama Mjane akiweka udongo
Wachungaji wakisaidiana kushusha sanduku
Askofu Mwaisabila akiongoza ibada siku ya leo
                   Mhe. Rais akiosha mikono baada ya kuweka udongo
Humu ndimo mwili ulivyolala
                              Wachungaji wakisaidiana kushusha mwili
Mhe. Rais JK akiongea siku ya leo
Mhe Rais.
Mhe. Rais alipokuwa akiondoka
Mkandamizaji akienda sawa siku ya Leo
Mwalimu Mwakasege
Mhe. Peter Msigwa akisalimia siku ya leo
Mhe. Ngeleja
Bishop Kakobe
CHANZO SAM SASALI BLOG

Zitto alipua tuhuma nzito

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amedai kuwa kuna wimbi la utoroshaji mkubwa wa fedha haramu nje ya nchi kuliko fedha za msaada na uwekezaji kutoka kwa wafadhili.
Aidha, Zitto amedai kuwa makampuni makubwa saba kati ya kumi yanayoongoza kwa kutorosha fedha na kuzificha katika nchi ambazo zimeweka sera za unafuu wa kodi na zisizokuwa na sheria za udhibiti wa uingizaji na upatikanaji wa mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Zitto alisema kati ya makampuni makubwa matatu ya simu hapa nchini, mawili yanahusika na ukwepaji mkubwa wa kodi kwa kujisajili katika nchi za Uholanzi na Ubelgiji, hivyo kuepuka kulipa kodi walizotakiwa.
Zitto alizidi kufichua kuwa moja ya kampuni kubwa za madini iliyoko hapa nchini imesajili makampuni mengine tisa katika nchi hizo, huku moja ya kampuni kubwa ya madini ikihusishwa na utoroshaji huo mkubwa.
Alisema nchi wahisani hutoa misaada inayokadiriwa kufikia kiasi cha dola za Marekani bilioni 37 huku uwekezaji kutoka nje ukiwa ni dola za Marekani bilioni 40 kwa mwaka.
Akizungumza juu ya mkutano wa 10 wa umoja wa kamati za mabunge za hesabu za serikali kutoka nchi wanachama wa SADC, (SADCOPAC), unaofanyika jijini hapa, alisema kumekuwa na matukio mengi ya kutorosha fedha na rasilimali za taifa katika nchi nyingi, na kuitolea mfano Tanzania ambayo imekumbwa na matukio hayo kwa kiwango kikubwa.
Alisema kumekuwa na utoroshaji wa fedha za taifa kupitia uuzaji wa mazao ya biashara, huku watendaji wa serikali wakionekana kuzidiwa ujanja.
“Mwaka 2011 Tanzania iliuza nje ya nchi tani 80,000 za korosho ambapo soko letu kuu ni India.
“Lakini utashangaa kuwa India wenyewe walisema kwa mwaka huo walipokea tani 120,000 kutoka kwetu, na hii inaonesha kuwa tani 40,000 zilitoroshwa bila kulipiwa kodi wala Benki Kuu (BoT) haina taarifa nazo, hivyo hawawezi kuzirudisha nchini kwa kuhofia kubainika,” alisema.
Aliongeza kuwa Tanzania inapoteza asimilia tano ya pato la ndani la taifa (GDP) kwa usafirishwaji wa fedha haramu zinazotokana na ukwepaji wa kodi na rushwa ambayo ni sawa na zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.25 kila mwaka.
Aidha, amesema kuwa  kiasi cha zaidi ya dola za Marekani bilioni 844  zimekuwa zikitoroshwa nje ya Bara la Afrika kila mwaka kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2000 mpaka 2010  wakati misaada kutoka nchi wahisani na uwekezaji kutoka nje (FDI) zikikadiriwa kufikia kiasi cha dola za Marekani bilioni 80 kwa mwaka.
“Theluthi mbili ya fedha haramu hutoroshwa kwa kughushi nyaraka za malipo kwa kuongeza au kupunguza gharama halisi ya bidhaa wanazosafirisha nje au kuingiza barani Afrika ambapo kila dola moja inayokuja Afrika kama msaada dola saba hutoroshwa kwa njia haramu,” alisema.
Alifafanua kuwa sheria za nchi hizo, hazimlazimishi mtu ama kampuni kutoa maelezo ya namna alivyopata fedha hizo, na kama analipa kodi sahihi, jambo linalowavutia watu na makampuni yasiyo na uaminifu kuficha fedha hizo huko.
Zitto alisema kwa kuwa matukio ya aina hiyo yamesababisha athari kubwa za kiuchumi, hivyo ni jukumu la kamati za mahesabu ya umma kwenye kila nchi kufanya kazi ya kudhibiti utoroshwaji wa fedha haramu huku akiainisha changamoto iliyopo kwenye baadhi ya nchi za Afrika ambazo hazina kamati hizo, na zile zilizonazo za muda tu, kama Zambia na Swaziland.
Kutokana na hujuma hizo, wajumbe wa mkutano huo wanaokadiriwa kufikia 300 wamewasukumia lawama wabunge wa nchi nyingi za Afrika kwa kuweka mbele masilahi ya vyama vyao vya siasa  badala ya masilahi ya wananchi.
Mbunge wa Afrika Kusini, Nikiwe Num, wakati akichangia mada kwenye mkutano huo wa kamati za usimamizi wa hesabu za serikali za nchi za Kusini mwa Afrika (SADCOPAC), alisema lazima wabunge wazibane serikali zao kikamilifu, vinginevyo wimbi la hujuma litaongezeka.
Ameongeza kuwa kama wabunge hawatabadilika, wataendelea kulalamika tu, badala ya kuchukua hatua dhidi ya watawala na kuweka kando tofauti zao za kiitikadi.
“Mataifa ya Afrika yana katiba nzuri sana, tatizo hazifuatwi na tukiendelea kuweka mbele masilahi ya vyama hatutaweza kuzisimamia serikali kwani wabunge wengi wanatoka kwenye vyama tawala kila mara tutakuja hapa tukilialia kuwa mambo hayaendi lazima tubadilike,” alisema Num.
Awali Mwenyekiti wa SADCOPAC, Sipho Makama, kutoka nchini Afrika Kusini alisema kuwa mkutano huo unazikutanisha nchi zote za SADC isipokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo kwa sasa hali si shwari nchini humo kutokana na vita inayoendelea kati ya serikali na waasi wa M23.
Zaidi ya wajumbe 300 wanahudhuria mkutano huo ambao ni wabunge wa kamati za hesabu za serikali, wakaguzi na wadhibiti wa hesabu za serikali, wahasibu wakuu wa serikali, makatibu wa kamati za PAC, maspika wa mabunge ya SADC pamoja na wahisani kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa.
chanzo-Tanzania daima