Idadi ya waliofariki yakia kumi.
Miili ya watu waliofariki kutokana na mapigano ya kugombea ardhi baina
ya wakulima na wafugaji katika hifadhi ya jamii ya Emboley Mortangosi
wilayani Kiteto mkoani manyara, imeongezeka zaidi kutoka sita
ilizopatikana juzi na kufikia jumla ya kumi.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi Akili Mpwapwa amesema, nyumba
zilizochomwa moto ni zaidi ya thelethini ambazo ni za wakulima.
Mapigano haya baina ya wakulima na wafugaji katika hifadhi ya jamii ya
Emboly Mortangosi wilayani Kiteto kwa kipindi hiki, yametokea baada ya
mkutano wa mkuu wa mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo, alioufanya wiki
iliyopita, kuwataka wakulima na wafugaji waliovamia hifadhi hiyo
kuondoka ikiwa ni agizo la mahaka ya Rufaa.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi Akili Mpwapwa amesema, mapigano hayo
yamezuka kwa wafugaji kuwashambulia wakulima na kuwaua pia kuchoma moto
nyumba zao.
Mgogoro baina ya wakulima na wafugaji katika
hifadhi ya Emboley Mortangosi wilayani Kiteto Mkoani Manyara, ulianza
mwaka 2006 baada ya halmashauri ya wilaya hiyo, kuwaamuru wafugaji na
wakulima waliovamia hifadhi kuondoka.
Wafugaji wamekuwa
wakiwashambulia wakulima kwa kile kinachosemekana, wanadai wanastahili
kuendelea kuishi katika hifadhi kwa kulisha mifugo yao ambayo haiharibu
mazingira.
MWISHO
No comments:
Post a Comment