Sunday, January 12, 2014

R.I.P Ariel Sharon

MUngu amlaze mahala pema peponi Ariel Sharon, shujaa mwerevu akeshae Hodari mwepesi na risasi zake hazikosi shabaha! Huyu Ariel Sharon ndiye aliyetufanya sisi wakristu tuende kuhiji Jerusalem na betlehem bila kuvaa hijab wala misuri na kuwekewa sheria kali za kidini.

Huyu ndiye yule shujaa aliikomboa jerusalem kutoka mikononi mwa wahamiaji haramu wa kipalestina. Kumbuka jerusalem ni Jiji la mfalme David. Ushujaa wa Sharon sio tuu ulimpendeza Adan na Eva bali pia mababu na mambu wa israel waliowahi kuwa wafalme .

Sharon kapigana vita vyote saba ya kuikomboa Israel tangia alipokuwa ana umri wa miaka 18 mwaka 1946 mpaka uhuru wa israel mwaka 1948. Vile vile alipigana vita vyote vya kuilinda Israel na kuhakikisha mwarabu hakanyagi Jiji takatifu la Jerusalem. Ili kulinda uhai wa raia wa kiisraeli na mali zao, alihakikisha sheria ya jino moja kwa meno nane.

Sharon ndiye meja jeneral aliyeuteka mfereji wa suezi kanali kwa masaa mamtu tuu akiwa mbioni kuingia cairo mpaka UN ikaingilia kati.

Sharon hakuwa na chuki na waarabu kabisaa ila yeyey alitaka sana kukomesha ugaidi tuu na kuwaletea maisha bora ya usalama waisraeli nchini mwao.

Huyu ndiye meje jeneral aliyeteka ardhi nyingi za waarabu na kuhakikisha atazirudisha kwa mkataba wa amani.

Sharon, aliongoza kikosi cha kuwatimua settlers wote wa ki Israel katika jangwa la sinai na Ukanda wa Gaza ili kuleta amani nchini Israel.

Kwa kweli mtu huyu alikuwa shujaa wa amani na usalama wa taifa la mungu.

Hakika mtu huyu kampendeza mungu na watu wenye mapenzi mema. He is at the right hand of the father together with Mama Teresa, Sokoine, Keneddy, Mandela and all saints.

No comments:

Post a Comment