Friday, October 5, 2012

Mazishi ya Kardinali Rugambwa Bukoba yarindima

MAELFU ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya nchi, wamefurika kwa wingi mjini hapa kuhudhuria mazishi ya Kardinali wa kwanza Mwafrika, hayati Kardinali Laurian Rugambwa aliyefariki takriban miaka 15 iliyopita.
Mazishi haya yaliyovuta watu wengine wakiwemo wa madhehebu na dini nyingi, yataenda sambamba na maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa Kardinali huyo pamoja na sherehe za kutabaruku Kanisa Kuu ambalo limejengwa upya la Bikira Maria mama wa Huruma.
Karibu mitaa yote imejaa watu, na nyumba zote za kulala wageni, seminari na sehemu nyingine zimejaa watu, wakiwemo wafanyabiashara wa vyakula, mapambo, mavazi, vitabu na vifaa vingine vya kikanisa, wakiwa miongoni mwa waliofika mjini hapa.
Kutokana na wingi wa watu, ratiba za ndege zimeongezeka kutoka safari moja, huku idadi ya mabasi na magari madogo yaliyojaa watu wanaokuja katika tukio hili ikizidi kuongezeka kila siku.
Hali ya ulinzi imeimarishwa zaidi, huku askari polisi wakionekana kuweka doria karibu kila barabara na mtaa wa mjini hapa.
Taarifa kutoka katika uongozi wa kanisa zimebainisha kuwa serikali itawakilishwa na Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal, huku baadhi ya maaskofu na viongozi wengine wa juu wa dini na madhehebu mengine wakiwa miongoni mwa waliokwishawasili mjini hapa tayari kwa tukio hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya ibada hiyo, ibada ya misa katika Parokia ya Kashozi alikozikwa, itaanza majira ya saa 5:00 hadi saa 8:00 mchana, kisha yatafuatia maandamano ya kuupeleka mwili huo katika kanisa kuu mjini Bukoba kuanzia muda huo hadi saa 9:30.
Ibada rasmi ya mazishi itaanza saa 9:30 hadi 10:30. Mnamo majira ya saa 11:30 jioni kutakuwa na ibada ya masifu kuashiria kukamilika kwa shughuli nzima za mazishi.
Saa 8-9.30 maandamano kuelekeza kanisa kuu na saa 8:30-10:30 misa ya mazishi, saaa 10:30 – 11:30 masaifu ya jioni.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa kesho Jumapili, ibada ya misa takatifu ya kutabaruku kanisa kuu jipya itaanza saa 3:00 asubuhi na kuendelea hadi saa 8:00 mchana ambapo wimbo maalum usemao ‘Mahali Hapa Panatisha Sana’ (Mwan 28:17) uliotungwa na mtunzi maarufu

No comments:

Post a Comment