Friday, April 22, 2016

HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17.

Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Januari, 2016
_________________________________
1. SHERIA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA MAWAZIRI (MINISTERS – DISCHARGE OF MINISTERIAL FUNCTIONS – ACT, 1980.
Mheshimiwa Spika, kifungu cha 5(1) kinaweka masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali yake.
Inasomeka ifuatavyo: Nanukuu “the President shall from time to time by notice published in the Gazette, specify the departments, business and other matters and responsibility for which he has retained for himself or he has assigned under his direction to any minister and may in that notice specify the effective date of the assumption of that responsibility…….” mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Serikali inafanya kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake na kazi kwa wizara mbalimbali. Hii ina maana kwamba Serikali inafanya kazi kwa kauli za Rais na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote wenye msingi na uhalali wa kisheria.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa mwongozo wa utendaji wa Serikali kwa kila Wizara (Instrument) unaotumika ni ule uliochapishwa kwenye gazeti la Serikali namba 494A la tarehe 17/12/2010. Kwa mujibu wa Instrument hiyo, majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni:
Coordination of Government Business
Leader of Government Business in the National Assembly
Link between Political Parties and Government.
National Festivals and Celebration of Management of Civic Contingencies (relief).
Facilitation and Implementation of Plans for the Development of Dodoma as Capital of Tanzania.
Coordination and Supervision of Transfer of the Government to Dodoma.
Government Press Services.
Investment, Economic Empowerment, Public-Private-Partnership (PPP), Poverty alleviation Policies and their Implementation.
Facilitation of the Development of Informal Sector.
Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office
Extra – Ministerial Department, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT:
Decentralization by Devolution (D by D), Rural Development, Urban Development Policies and their Implementation.
Regional Administration.
Primary and Secondary Education Administration
Dar Rapid Transit – DART.
Performance Improvement and Development of Human Resources under this Office.
Extra-Ministerial Departments, Parastatal Organisations, Agencies, Programmes and Projects under this Office.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali hii kuendesha kazi zake kwa Mwongozo wa 2010 ina maanisha kwamba majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu bado ni yale yale yaliyochapishwa mwaka 2010, kwa sababu gazeti hilo la Serikali halijafutwa.
2. UVUNJWAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI KUHUSIANA NA BAJETI UNAOFANYWA NA SERIKALI
Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge la Bajeti ambalo kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepewa mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaaka wa Bajeti kwa madhumuni ya kujadili na kuidhinisha Bajeti ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, Ikiwa fedha zilizoidhinishwa na Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya Serikali , kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba: “ Serikali itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji ambayo hayakupangwa”.
Mheshimiwa Spika utaratibu huu unatiliwa nguvu na Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka 2001( Public Finacne Act, 2001)ambapo kifungu cha 18 (3) na (4) kinaitaka Serikali kuleta Bungeni bajeti ya nyongeza ( mini-budget) kwa ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha zilizoidhinishwa awali hazikutosha.
Mheshimiwa Spika, utaratibu huo wa kisheria umekuwa ukivunjwa na Serikali kwa kufanya matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na Bunge jambo ambalo linaua dhana ya madaraka ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri Serikali.
Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha jambo hilo, kwa mfano bajeti ya maendeleo iliyokuwa imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2015/16 ilikuwa ni shilingi bilioni 883.8 ambapo kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni shilingi bilioni 191.6
Mheshimiwa Spika, Jambo la kushangaza ni kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.
Mheshimiwa Spika, ukitazama takwimu hizo utaona kuwa kuna ongezeko la fedha zilizotolewa na hazina hadi kufikia mwezi Machi 2016 ukilinganisha na fedha zilizoidhinishwa na Bunge. Tangu kuidhinishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya nyongeza iliyoletwa Bungeni na Serikali kwa ajili ya kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria ya Bajeti ya 2015 au sheria ya Fedha ya 2015.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali kuamua kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.
3. UHURU NA MADARAKA YA MHIMILI WA BUNGE
Mheshimiwa Spika, Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalitaja Bunge kuwa ndicho chombo kikuu katika Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Katika hali isiyo ya kawaida, kifungu hiki cha Katiba kimevunjwa na badala yake Serikali imelipoka bunge madaraka yake na Bunge kwa maana ya uongozi wake wanaonekana kushiriki na kukubali kupokwa huku kwa madaraka na uhuru wake.
Mheshimiwa Spika, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki ya kujua Bunge lao linavyofanya kazi ili wawe na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao iwapo hawafanyi kazi inavyostahili. Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali na uongozi wa Bunge, imewapoka wananchi haki yao ya kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala Bungeni kurushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya habari vya kujitegemea.
Mheshimiwa Spika, Jambo hili pia ni uvunjwaji wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo inasema kwamba kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake; anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake na anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii,
Mheshimiwa Spika, katika Mazingira kama hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiko tayari kuendelea kushiriki uvunjaji wa Katiba Sheria na haki za msingi za wananchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake katika mazingira haya na inaushauri uongozi wa Bunge kupata ufumbuzi wa haraka wa kadhia hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za msingi za wananchi. Hivyo basi Kambi bado inatafakari kwa kina na makini hatua za kufuata.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI
KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU
22 Aprili, 2016.

Utajiri wa Mwanasiasa mtata wa Marekani Donald Trump-Jamaa anazo pesa hasa.

Najua kuna watu wangu mnafuatilia mchakato wa uteuzi wa kumpata mgombea urais Marekani. Dolnad Trump ni moja ya wagombea wa Republican ambao wamechukua headline sana na anaonekana kama kuelekea kufanikiwa hivi, usishangae ikaishie anaingia white house.
Mwanasiasa huyu mtata amezaliwa sehemu ambayo wazazi wana pesa, lakini mali zake zimekuwa zikiongezeka kutokana na biashara zake, sasa ana miaka 69 na ana utajiri wa unaokadiriwa kufika  Dola bilioni 8.7 kwa takwimu za june 2015. 
Donald Trump alianza kufanya kazi kwenye kampuni ya baba yake na akanza kupiga mpaka deal kubwa ukitaka kuufahamu zaidi utajiri wa mwanasiasa huyu na billionare angalia picha hizi hapa chini.
1
Enzi za ujana wake Donald 
2
Akionekana na helkopita yake mwenyewe
3
Hii ni moja ya Uwanja wake wa Gofu uliopo Washington DC
5
Ndege yake aina ya Boeing 727-23
6
muonekano wa ndege kwa ndani
7
.
8
.
9
.
10
.
11
Donald Trump na Mkewe Melania Knauss Trump
12
Mjengo wa Donald Trump
13
Muonekano wa Ndani wa mjengo wa Trump
14
.
15
Hili ni eneo lake jingine la kuishi, Palm beach Florida
16
Hili ni eneo la Swimming pool kwenye nymba yake ya kuishi
17
hapa ni nyumba ya zamani ya Trump
18
Huu ni mwonekano wa ndani wa nymba ya Trump ya zamani
19
Ukumbi wa Cinema kwenye mjengo huo 
20
Unaweza ukaangalia moja muonekano wa Dining room kwenye mjengo wake huo wa zamani

JPM TUPIA JICHO MFUMO WA ELIMU NCHINI, NI "JIPU" KUBWA ZAIDI YA UDHANIAVYO.!-By Malisa GJ,

Kati ya vitu navyotamani sana kuona vikifanyika ni marekebisho makubwa ya mfumo wa Elimu Nchini. Natamani kuona shule za sekondari za serikali zikirudishwa ktk hadhi yake. "Special schools" ziwe "Special" kweli. Tuone watoto wetu wakipambana kwenda Ilboru, Kibaha, Tabora boys, Mzumbe etc. Sio kupambana kwenda St.Marry's au St.Francis.

Nakumbuka miaka 21 iliyopita kaka yetu alifaulu darasa la 7 kwenda sekondari ya Iyunga (Mbeya) akitokea kule kijijini Old Moshi. Wakati tunamsindikiza kupanda basi alikua anatupa hamasa ya kusoma ili tufanye vizuri zaidi yake. Kipimo kilikua kwenda "special school".
Nakumbuka matokeo ya darasa la 7 au kidato cha 4 yalikua yakitoka tunaenda kujazana ofisi za Halmashauri ya wilaya kuangalia umepangwa wapi. Ruvu, Kigonsera, Kantalamba, Ndanda, Pugu, Magamba, Mwenge, Same, Mazengo au Mzumbe?
KWA WAVULANA: Tabora boys, Songea Boys, Bwiru boys, Nsumba, Lyamungo, Umbwe etc.
KWA WASICHANA: Weruweru, Ashira, Songea girls, Nganza, Loleza, Iringa girls etc.
Zilikuwepo shule za ufundi ambazo zilichukua watu wa daraja la pili la Ufaulu. Yani shule za vipaji ndio zilichukua wale "bright" waliofuata wakaenda shule za Ufundi kama Tanga Tech, Iyunga Tech, Mtwara Tech... Waliofuata wakaenda shule za kawaida za Boarding kama Pugu, Ruvu, Galanos etc.
Waliofuata wakaenda shule za kutwa (day school), ambazo nazo hazikuwa mchezo kupata nafasi. Nakumbuka mdogo wangu alipata alama 120 kati ya 150 yani wastani wa daraja A ya asilimia 81% lakini alipangwa day school (Mawenzi).
Zilikuwepo pia shule maalumu kwa ajili mchepuo wa biashara. Yani ukipita huko unajiandaa kuja kusomea Uhasibu, Masoko, au biashara kwa siku za baadae. Shule kama Umbwe na Shycom zilikua maalumu kwa michepuo ya ECA, EGM etc.
Kwa ujumla serikali ilikua imejipanga vizuri sana ktk sekta ya Elimu. Kuanzia ngazi ya chini kabisa kwa shule za msingi hadi Elimu ya juu.
Na ilitumia mfumo mzuri wa kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao. Kwa mfano mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA yalisaidia sana kuinua kiwango cha Taaluma na michezo. Wanafunzi walishindanishwa ktk michezo na taaluma pia.
Nakumbuka nikiwa darasa la 6 nilishiriki mashindano ya somo la HISABATI na nikafanikiwa kufika hadi ngazi ya wilaya. Pale ninakutana na vichwa vya "number" nikachujwa japo nilipata 45 ya 50. Waliofanya vizuri wakaendelea ngazi ya mkoa na hatimaye taifa. Na mwishoni alipatikana bingwa wa Hisabati kitaifa.
Mashindano ya sanaa (uchoraji, uchongaji, kusuka etc). Mashibdano ya Insha (darasa la 4), mashindano ya Umahiri ktk lugha ya kiingereza (darasa la 5) ni moja ya mambo yaliyofanya wanafunzi kusoma kwa bidii na kuibua vipaji vyao.
Wengine kwenye michezo kama Riadha, Soka, kuruka viunzi, kukimbia na magunia.. Wenye ktk uimbaji.. kulikuwa na Mashindano ya kuimba (kwaya ya shule) mnatunga nyimbo za kutunza mazingira, kusifia Tanzania au kupiga vita magonjwa kama Ukimwi halafu mnapimwa kwa maudhui ya wimbo na mpangilio wa uimbaji wenu (tone, melody, rythim etc).
Unamaliza shule unakuwa "multi-purpose".. unajua vitu vingi kwa wakati mmoja. Darasani unajua, michezo unajua, sanaa unajua.. yani unaimarika afya ya mwili na akili.
Kila nikitafakari haya yote nawaonea huruma sana wadogo zetu waliopo shuleni. Hawajui zaidi ya wanavyosoma kwenye vitabu.. Na bahati mbaya vitabu vyenyewe vinaandikwa vikiwa na makosa mengi.
Mwamko wa elimu hakuna tena na taaluma imedumaa. Watoto hawaandaliwi kuzikabili changamoto za maisha. Watoto hawaandaliwi kupambana ktk kusaka maarifa. Wanaandaliwa kuona elimu ni kitu cha kawaida na yeyote anaweza kuipata.
Wakati nikiwa darasa la 5 nilikua nimekariri miji mikuu yote duniani, Marais wote wa Afrika (kwa wakati ule), sarafu za nchi zote za Afrika, Marais wa kwanza wa nchi zote za Afrika, vyama tawala vya nchi zote za Afrika, Baraza la Mawaziri lote la Tanzania nikiwa kinda wa miaka 11 tu, lakini nimepigwa na butwaa juzi kuona kupitia EATV (kipindi cha Skonga) mtoto wa kidato cha 4 anaulizwa mji mkuu wa Somalia akajibu 'Al Shabab'
Nikajiuliza huyu amefikaje form four? Tena shule ya serikali. Nikagundua Mfumo wetu wa Elimu uko "loose" na umeruhusu kila mtu kupita tu hata kufika chuo kikuu hata kama hajui kitu.
Hujiulizi inakuaje darasa lina nwanafunzi 70 halafu 69 wanafaulu kwenda sekondari anafeli mmoja tu. How comes? Wakati mimi namaliza darasa la 7 tulikua wanafunzi 97 darasani. Tuliofaulu kwenda sekondari ni 6 tu. Yani wavulana watano na msichana mmoja. Ikawa gumzo kijijini kwamba tumefaulu wengi maana ilikua imezoeleka ni wawili au watatu.
Lakini leo hata asiyejua kusoma yupo sekondari. Na akitaka anafika hadi chuo kikuu. Unabisha?? Nenda UDSM, Mzumbe, SAUT au UDOM fanya "rundom sampling" upate mwanafunzi mmoja kisha mwambie akutajie jina la sarafu ya Zambia, Rwanda, Namibia, au Congo. Kama asiposaidiwa na "Google" nakuhakikishia atapata sifuri.
Au muulize akutajie marais wa kwanza wa nchi 5 za Afrika Mashariki.. Yani Rwanda, Kenya, Uganda, TZ na Burundi. Akijitahidi sana atakutajia Nyerere na Mzee Kenyatta. Wengine hadi asaidiwe na "google".. wadogo zetu hawasumbui tena vichwa kusaka maarifa.. wao busy "instagram, facebook na whatsapp" kila saa wanatupia picha.
Hizi simu wa gezitumia vzr zingewasaidia sana kusaka maarifa lakini hawana muda huo. Wanataka kuona "mastaa" wa bongo movie wanasema nini Insta. Wako busy kufuatilia maisha ya Diamond na Zari kuliko kufuatilia masomo.
Elimu yetu imefubaa... Elimu yetu imedumaa.. Elimu yetu inaugua kiharusi.. Tunahitaji kuchukua hatua madhubuti kuiokoa ili irudi ktk hali yake ya awali.
Bahati mbaya Viongozi wetu wamerahisisha sana elimu na ikaonekana ni kitu "cheap". yani elimu ni haki ya la kila mtu anayetaka.. Hata kama huna uwezo lakini ukitaka degree unaipata tu.. ili mradi uwe na fedha..
Ndio maana leo kuna vyuo vinatoa degree vipo jirani na garage, au stand za mabasi.. Unasikia chuo kinatangazwa kwenye vyombo vya habari kwamba kinatoa degree au diploma lakini kipo karibu na soko la Mitumba, au jirani na kituo cha daladala, mkabala na gereji au nyumba ya kulala wageni.
Na wanaotoka hapo wanaitwa wasomi. Wana vyeti vinavyopendeza sana. Wana GPA nzuri sana. Lakini wape kazi wafanye au wapime katika maarifa waliyonayo. Utajiuliza hivyo vyeti walisomea au wameviokota?
Mfumo wa Elimu duniani kote unapaswa kuwa pembetatu.. Yani wanaoanza ni wengi lakini kadri wanavyoenda juu idadi inapaswa kupungua. Kama shule za msingi wanafunzi ni laki 5 basi sio wote watakaoenda sekondari. Kama mwanafunzi hana uwezo wa kwenda sekondari atafutiwe shughuli nyingine ya kufanya. Sekondari waende wenye sifa na uwezo tu.
Na watakaoenda sekondari si wote watahitimu.. wengine watachujwa kidato cha pili wakatafute shughuli za kufanya.. wengine wataendelea lakini wakifika kidato cha 4 si wote watakaoenda kidato cha 5. Hivyohivyo hadi chuo kikuu.
Chuo kikuu sio haki ya kila mtu na haipaswi kuwa haki ya kila mtu. Ni kwa "wateule" wachache tu. Vyuo vya kati (Polytechnic) vinapaswa kuwa vingi maana ndio vinatoa watendaji lakini vyuo vikuu vinapaswa kuwa vichache maana vinatoa wasimamizi (managers). Na hivi ndivyo Mwalimu Nyerere alivyofanya.
Kwa mfano vyuo vya Ufundi vilikua vingi lakini chuo kikuu kimoja. Kwahiyo kama kuna kampuni ya Ufundi umeme unakuta Kuna Electrical Engineer mmoja mwenye degree huyu anakuwa Meneja. Halafu chini yake kuna mafundi sanifu (Technicians wa level za diploma), halafu chini kabisa kuna mafundi mchundo (Artisan) wa level za certifice kutoka VETA au vyuo vingine vya ufundi.
Kimsingi "mafundi sanifu" na "mafundi mchundo" ndio watenda kazi. Hawa ndio wanaingia "field". Kwahiyo "degree holder" yeye anawasimamia tu ili wafanye kazi inavyotakiwa.
Kwa kawaida "degree holders" wengi wanajifunza kwa nadharia zaidi si vitendo (isipokuwa kwa baadhi ya course kama MD, Law, Journalism etc). Kwa hiyo ukiwa degree holder wewe ni msimamizi (manager). Unajua kitu kinatakiwa kifanyikeje lakini hufanyi wewe. Kwa hiyo unawekwa msimamizi kusimamia wengine wafanye.
Lakini siku hizi imekuwa vice-versa. Unakuta kampuni ya umeme ina degree holder 18 wa Electrical Engineering na Diploma holder wawili. Sasa hapo nani anaingia "field?", nani anamsimamia, nani anasimamiwa?
Na tatizo lilianza baada ya serikali kurahisisha elimu na kuona ni haki ya kila mtu. Vyuo vyote vya ufundi daraja la kati vilivyokuwa vikitoa Technician wazuri kama Mbeya Tech, DIT na Arusha Tech vikageuzwa kisiasa na kuanza kutoa degree. Kwahiyo wahitimu wa DIT wakimaliza hawashiki tena spanner maana wao sio "Technicians" tena. Wana degree kwahiyo nao wanataka kuvaa tai au suti wakae kwenye viyoyozi.
Mfumo wetu wa Elimu umepinduka miguu juu kichwa chini. Wanaojiita wasomi wa "Degree" (managers) wamekuwa wengi kuliko wasomi wa taaluma za kati (implementers). Na hii ni tatizo kubwa. Huwezi kuwa na Managers wengi kuliko watendaji. Wanam-manage nani sasa?
Ukiona taifa lina wasomi wengi wa vyuo vikuu na upungufu wa wasomi wa vyuo vya kati ujue taifa hilo halizalishi. Limedumaa kwa sababu Wanaofanya uzalishaji ni wataalamu wa ngazi za kati. Wasomi wa vyuo vikuu ni wasimamizi tu. Sasa tumefanya kila mtu kuwa msimamizi, je nani awe mzalishaji?
Ndio maana Wachina wakija kujenga barabara wanakuja na mafundi sanifu (Technicians) kutoka kwao halafu tunaanza kulalamika kuwa ajira zetu wanapewa wageni. Mnalalamika nini wakati mafundi sanifu hakuna? Vyuo vya kutengeneza mafundi sanifu mmevigeuza vyuo vikuu, sasa hivi vinazalisha wasimamizi (managers) badala ua kuzalisha watendaji?
Nchi hii ina vyuo vikuu kama utitiri. Ukipitia taarifa ya TCU na ukapitia ya NACTE utagundua nchi hii ina vyuo 64 vinavyotoa elimu ya juu kwa ngazi za "degree" na kuendelea. Vingine ni "Universities" vingine ni "Non university institutions".
Hivi vyuo vyote hivi vinatoa elimu kwa ubora unaotakiwa? Sina shida na idadi ya vyuo ila standard ya elimu inayotolewa huko. Tunazalisha wasomi wa viwango vya kukubalika kimataifa? Au tumetanua goli kila mtu apite.?
Nilienda Songea nikakuta Chuo kikuu kinaitwa St.Joseph (nashukuru serikali imeshakifunga) yani nikasikitika sn. Chuo kikuu kinazidiwa majengo na shule ya msingi Vingunguti A??
Chuo hakina maabara, hakina maktaba, hakina hostels, hakina sifa hata ya kuwa shule ya sekondari. Labda shule ya msingi kwa shida. Lakini ni chuo kikuu na wadogo zetu walipelekwa huko na TCU.
Vipo vyuo vingi vya aina hii. Serikali ifanye ukaguzi upya ivifunge. Heri tuwe na vyuo vichache vyenye "standard" ya kueleweka kuliko kuwa na mavyuo mengi yasiyo na tija. Kuna haja gani ya mwanafunzi kujiita ana degree wakati hata CV hawezi kuandika?
Juzi nilikuwa kwny pannel ya usaili wa nafasi fulani za kazi nikamwambia mmoja wa wadahiliwa ajieleze kwa dakika mbili lakini akaishia kutaja jina lake na umri wake tu. Mwingine akataja degree yake (Business Information System) tukamuuliza hiyo degree ni ya Social science, Pure Science au Business afiliated? Akashindwa kujibu akaomba kuangalia kwenye cheti chake imeandikwaje. Nikashangaa lakini nikamuonea huruma. Ina maana miaka mitatu alisoma kitu asichokijua vzr? Kwa hali hii ni ngumu kushindana kimataifa.
Nina mengi ya kusema lakini ukurasa huu hautoshi kuandika yote.. Itoshe tu kusema Mfumo wa Elimu nchi hii unahitaji marekebisho makubwa sana ya kimfumo. Natamani kuona Magufuli akiumizwa na hili la elimu kama anavyoumizwa na "majipu". Mfumo wa elimu wa nchi hii ndio jipu kubwa zaidi. Tumshauri Rais alitumbue kwa gharama yoyote ile.!
Malisa GJ.!

UONGO,UZUSHI NA UKWELI KUHUSU SIMU ZA MKONONI-YONA FARES MARO

Umewahi kusikia , kusoma na kutazama uwongo mwingi kuhusu simu za mikononi . lengo la makala hii ni kujibu uwongo huo na kutoa ufafanuzi kidogo kwa baadhi ya mambo muhimu .
Simu za mkononi zina mionzi sana , kwahiyo usiweke sehemu nyeti kama katika mifuko ya suruali au shati . Ukweli ni kwamba simu nzuri lazima ipitie majaribio yanayoitwa SAR (Specific Absorption Rating) . Inapokua dukani ina maana imepitia huko na kuthibitishwa ubora wake .
Pia hakuna uhusiano wa matumizi makubwa ya simu na magonjwa uliothibitishwa kisayansi .
Simu ikiwashwa ndani ya ndege inaweza kuingiliana na mitambo ya kuongozea ndege na ni hatari kwahiyo zimezuiwa .
Unachotakiwa kujua ni kwamba mitambo ya kisasa ya mawasiliano na kuongozea ndege imeboreshwa sana . hata ndege iliyojaa watu wote wanaotumia simu za mikono hawata sababisha madhara yoyote .
Kama simu yako ingekua hatari kihivyo basi ungetakiwa kuiacha chini usipande nayo wakati wa ukaguzi au wakati wa taratibu nyingine . Sababu ya kwanini hutakiwi kutumia simu ni ili kuweza kudhibiti abiria na ili uweze kusikiliza matangazo ya mara kwa mara maana usafiri wa ndege unajulikana changamoto zake .
Simu zinaweza kusababisha moto au milipuko katika vituo vya mafuta .
Petroli na mafuta ya aina nyingine yanaweza kuwashwa kwa cheche tu . Lakini cheche inaweza kutoka katika kiberiti , viwashio au hitilafu za umeme ila sio kutoka kwenye simu yako . Hofu iliyopo ni kwamba simu yeye tatizo au betrii inaweza kusababisha cheche na moto lakini hii ni ngumu na hakuna matukio kama hayo yaliyowahi kuripotiwa .
Hautakiwi kuchaji simu usiku mzima : itafupisha maisha ya betrii na kuharibu kifaa chako . Mimi huwa nachaji simu usiku wakati wa kulala lakini huwa nazima .
Hata hivyo unatakiwa kujua kwamba , vifa vyote vya kisasa vyenye betrii huwa na soketi ndani inayozuia isijichaji zaidi kwahiyo kuzuia uharibifu wowote . Betri ikishajaa , itaacha kujichaji yenyewe . Lakini kifaa kinaweza kuendelea kupeleka moto kutokana na sababu kadhaa haswa kama simu imewashwa ikiwa labda inapigwa sana au inafanya shuguli nyingine .
Hapo rejea kwenye suala la kununua vifaa orijino maana vitaweza kukuepusha na matatizo kama hayo .
Ukubwa wa Betrii maana yake betrii itakayodumu zaidi .
Iwe laptop , simu ya mkono au kifaa chochote kinachotumia betrii , uhai wa betrii unahusiana na jinsi kifaa kinavyotumika haswa kwenye suala la umeme .
Unaponunua kifaa chako kikiwa kipya soma makaratasi ya maelezo au ingia katika mtandao utasoma mengi kuhusu utunzaji wa kifaa chako na utadumu nacho kwa muda mrefu .
Utumiaji wa Intaneti kutumia simu ya mkono ni salama zaidi kutoka kwa wahalifu na watu wengine wanaokufuatilia .
Kila simu ina Kivinjari ( Browser ) yenye kitu kinachoitwa incognito mode yenye kuweza kukufanya uwe kibinafsi zaidi lakini hii inazuia kuacha historia isijihifadhi katika kifaa chako . Haitaweza kuficha majina yako , ulipo sasa hivi , shuguli unazofanya , tovuti au blogu ulizotembea , haiwezi kukuficha kutoka kwa polisi au wamiliki wa huduma ya mawasiliano unayotumia kama ni VODA , AIRTEL , TIGO , TTCL .
Usipige simu wakati simu yako iko kwenye chaji kwa sababu inaweza kulipuka .
Ni kweli kwamba kumewahi kutokea matukio kadhaa ya simu na vifaa vingine kulipuka , lakini ni betri za vifaa husika ndizo zinazosababisha moto na kulipuka sio kifaa chenyewe .
Kwababu simu au betri inaweza kuwa feki na yenye kiwango kidogo cha ubora , au ni zile zilizotumika na kuuzwa tena . Kama ukitumia betrii na chaji original kwa jinsi unavyotakiwa kutumia hautapata matatizo kama hayo hata kidogo .
Kwa suala hili , tujihadhari na simu za mikononi tusizojua ubora wala zilikotoka maana matatizo huanzia hapo .
Kwa kuwa TCRA imetangaza kufungia simu feki baadaye mwaka huu , naamini kutakua na simu za maana mitaani na matatizo kama haya yanaweza kupungua kwa kiasi kikubwa kama sio kuisha kabisa baada ya muda mfupi .
Nakutakia matumizi salama ya kifaa chako cha mawasiliano kwa ajili ya kuzalisha , kujenga uchumi , upendo , amani na mshikamano lakini sio kinyume chake .
Mwisho napenda kusema kwamba sifanyi kampuni yoyote ya simu wala sihusiki na biashara yoyote inayohusu simu kwahiyo sina maslahi yoyote katika somo hili zaidi ya kuona wenzangu wanaelimika na kuondoa hofu .
YONA FARES MARO
0786 806028

Youth Night Live kufanyika leo tarehe 22 mwezi wa nne 2016 katika ukumbi wa New Life Outreach-( Kwa Egon Sakina )


( Kwa Egon Sakina )
Youth Night  live ni maalum kwa vijana kwaajili ya kuwamsha kiuwezo na akili zao pia kuwafanya waweze kuamka kiroho ili wawe chachu  ya maendeleo ya kanisa na taifa kwa ujumla.

Imekuwa kwa vijana kwa sababu vijana ndio nguzo ya taifa na kanisa, vijana watarajie kubadilika na pia kukutana na Mungu, kutakuwa na maombezi maalum ya vijana katika sehemu mbalimbali za maisha yao na kuombea taifa kwa ujumla.Watakuwepo viongoozi wa serikali na wa kanisa pia maaskofu na wachungaji watakuwepo.

Walimu nao watakuwepo akiwemo Shemeji Melelayeki, Emmanuel Mkwaya, Fred Chavala na Filex Ntambara toka Uganda.

Vikundi vitakavyo hudumu katika usiku huu wa vijana watakuwepo Shangwe Voices, PCASF Praise Team, Rhema Worship Team, New Life Band na Abednego &The Worshipperz intl.

Tukio hili litarushwa live online radio ya Arusha Mambo FM unaweza kupakuwa(Download) Tunein kisha tafuta Arusha mambo.Kijana usipange kukosa  usiku huu.
Pia blogger wengi tutakwepo kukuhabarisha live toka eneo la Tukio.

Thursday, August 20, 2015

Albino 5 Tz warejeshewa viungo Marekani-Kwa hisani ya watu wa Marekani.

Mshirikishe mwenzako
Albino 5 raia wa Tanzania waliokatwa viungo wamerejeshewa viungo bandia Marekani
Watoto watano wa Tanzania wenye ulemavu wa ngozi waliokuwa wamekatwa viungo vya miili yao wamewekewa mikono na miguu ya bandia katika hospitali iliyopo nchini Marekani.
Watoto hawa ni miongoni mwa mamia ya watu wanye ulemavu wa ngozi nchini humo ambao wamekuwa wakiwindwa na watu wanaotaka viungo vya miili yao kwa shughuli za kishirikina
Watoto hao, mmoja wa kike na wanne wa kiume kutoka mikoa ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi mwa Tanzania, wamekuwa wakipokea matibabu hayo katika hospitali ya watoto Philadelphia Shriners Hospital iliyopo jijini New York.
Wanatarajiwa kurudi nyumbani Tanzania mnamo mwezi Septemba
Wakiwa na umri kati ya miaka 6 hadi 18, wanne wa watoto hawa walipatwa na majeraha makubwa ya kukatwa mikono na miguu yao, huku mmoja wao akiwa amekatwa taya na meno.
Tayari watoto wanne wamekwisha wekewa mikono na miguu ya bandia, wakati yule aliyekatwa taya akitarajiwa matibabu yake kuchukua muda mrefu zaidi
Shirika la msaada la Kimarekani Global Medical Relief Fund linafadhili matibabu ya watoto hawa.
Ofisa kutoka shirika la Under the Same Sun Martin Haule anasema watoto wanaendelea vizuri na kwamba ni wenye furaha
Shirika la Global Medical Relief Fund linafadhili matibabu ya watoto hawa.
Ameiambia BBC kwamba wanatarajiwa kurudi nyumbani Tanzania mnamo mwezi Septemba
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ulemavu wa ngozi unaathiri takribani mtu mmoja katika kila watu 15,000 nchini Tanzania.
Watu hawa wanawindwa kwa ajili ya viungo vyao, ambavyo vinatakiwa katika biashara haramu kwa matumizi ya shughuri za kishirikina
chanzo-bbc.com

WASIFU WA KINGWENDU KWA KIFUPI-NI MCHEKESHAJI MAARUFU NA MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CUF

KINGWENDU's PROFILE.!
Majina yake halisi ni Rashid Mwinshehe, na jina lake la kisanii ni "Kingwendu". Kabila ni Mzaramo mzaliwa wa Kisarawe. Elimu yake ni Stashahada ya Uhasibu (Diploma in Accounting) kutoka chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA).
Kitaaluma Kingwendu ni Mhasibu. Amefanya kazi ya uhasibu ktk taasisi mbalimbali kabla hajaamua kuachana nayo na kujiingiza kwenye sanaa za maigizo ambapo anafanya vizuri ktk sanaa za vichekesho (Physical and Character Comedy).
Kwa sasa anagombea Ubunge jimbo la Kisarawe kupitia chama cha wananchi CUF akiwakilisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Yeye mwenyewe anasema "mwaka huu CCM watageuka mapepe Kisarawe, wanaosema sijasoma waende TIA kuuliza records zangu.."
Alipoulizwa kwanini amechagua UKAWA na sio CCM kama wasanii wengine amesema "UKAWA ndio habari ya mjini, Ukijiunga UKAWA unapata raha duniani, aluu".