Thursday, August 20, 2015

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameapishwa kuanza muhula mpya



Katika hotuba yake, Bw Nkurunziza ameahidi kumaliza ghasia nchini mwake katika kipindi cha miezi miwili. Maafisa wawili wa ngazi ya juu, akiwemo mkuu wa zamani wa ujasusi wameuawa katika mashambulio tofauti mwezi uliopita, baada ya uchaguzi uliokuwa na utata. Mwanaharakati mmoja wa haki za binaadam pia alipigwa risasi na kujeruhiwa. Kulikuwa na jaribio la kumpindua Rais Nkurunziza mwezi Mei.

No comments:

Post a Comment