Thursday, August 20, 2015

Ninayo Ripoti toka China, hawa ndio waliokamatwa ndani ya mwezi mmoja kwa wizi mitandaoni

Cyber Crime enter key and handcuffs , full frame
Bado kama wiki moja na nusu kushuhudia Sheria ya Kudhibiti Matumizi ya Mitandao Tanzania ikianza kufanya kazi rasmi kabisa, hiyo ni kutokana na taarifa rasmi kabisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano TCRA.
Nimeipata Ripoti toka China, wao walianzisha kitu kinachoitwa ‘Operation Clean Internet’ ambayo ilianza mwezi July 2015, hii ni kwa ajili ya kupambana na wahalifu wa Mitandaoni.
cyber crime
Katika Upelelezi uliofanyika mpaka sasa kumekutwa matukio kama 7,400 ya uhalifu Mitandaoni inayohusishwa na kesi za ku-hack account za watu pamoja na Makampuni.
Mpaka sasahivi watu waliokamatwa China ni 15,000 kutokana na kutuhumiwa na kesi za kujihusisha na uhalifu kwa kutumia Mitandao , hiyo ni ndani ya mwezi mmoja tu toka waanzishe hiyo Operation maalum kabisa!!
Kwa kuanza kabisa kudhibiti hii kitu watu walitakiwa kuanzisha accounts Mitandaoni kwa majina yao kamili, pamoja na Bloggers wote kujisajili Serikalini.
source-Millady ayo.com

No comments:

Post a Comment