Saturday, June 7, 2014

DCI amkwepa Kibanda

MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Isaya MunguluMKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Isaya Mungulu, amekwepa kuzungumzia sakata la kutekwa, kuteswa, kutobolewa jicho na kukatwa kidole kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini, Absalom Kibanda.
Hali hiyo ilitokea jana, wakati Mungulu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo mwandishi wa gazeti hili alimtaka aeleze uchunguzi wa sakata la Kibanda umefikia wapi hadi sasa.
Tangu Kibanda atendewe unyama huo, Machi mwaka jana, hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa, na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu na Makao Makuu wamekuwa na majibu ya kukinzana.
Huku akijibu kwa kubabaika na akitaja sakata jingine la Dk. Stephen Ulimboka aliyetendewa unyama kama huo Juni mwaka 2012, Mungulu alisema: “Suala la Kibanda ni suala la ghafla, siwezi kulisemea kwa sasa.”
Vile vile Mungulu alikwepa kujibu swali jingine kuhusu malalamiko ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, aliyedai kuna askari walioshirikiana na wezi bandarini kuiba shaba kwa kutumia kichwa cha treni ya Tazara.
“Kwa suala la askari waliotuhumiwa kuiba naomba aulizwe Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ndiye mwenye askari hao,” alisema Mungulu.
Tanzania Daima lilimtafuta Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, ambaye alisema bado halifahamu, na kwamba itabidi asubiri kuona taarifa hiyo iliyoripotiwa ili aweze kuita mkutano na waandishi kulifafanua.
Awali Mungulu alizungumzia operesheni ya wakati mmoja kwa nchi za Afrika Mashariki, na nchi za Kanda ya Kusini mwa Afrika, iliyofanya Mei 29 na 30 mwaka huu.
Alisema operesheni hiyo imetokana na maamuzi yaliyofikiwa kwenye mkutano wa wakuu wa majeshi ya polisi wa kanda zote mbili ulioandaa kikao kilichowakutanisha wakuu wa upelelezi wa nchi hizo.
Katika kikao hicho kilichofanyika Machi 13 -14 nchini Namibia, suala la usafirishaji wa binadamu na wahamiaji haramu, dawa za kulevya, wizi wa magari, makosa ya wanyama pori, silaha haramu, usafirishaji wa madini na wizi wa nyaya za shamba ndiyo yalipewa kipaumbele.
Alisema kuwa kwa upande wa Tanzania baada ya operesheni hiyo, usafirishaji haramu wa binadamu ulipata wahamiaji 84, ambapo 77 waliotoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 7.
“Polisi wa Tanzania walikamata heroine gramu 5, bangi gramu 8 na misokoto 195, huku mirungi ikipatikana ya kilogram 200

No comments:

Post a Comment