Kundi la wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria limekana madai kutoka kwa serikali ya Nigeria kuwa wameafikia makubaliano.
Akizungumza kwa njia ya kanda ya video, kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau alisema kuwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara kutoka eneo la Chibok kaskazini mwa Nigeria wamebadili dina na kuwa waislamu na kwamba wameolewa.
Shekau amasema kuwa hakujakuwa na majadiliano yoyote na serikali ya Nigeria.
Kiongozi huyo wa Boko Haram pia alitumia ujumbe huo kuthibitisha kuwa wanamshikilia raia mmoja mjerumani ambaye anakisiwa kuwa mwalimu aliyetekwa nyara mwezi Julai.
Serikali ya Nigeria inasema kuwa mazungumo na kundi Hilo yanaendelea kwenye nchi jirani ya Chad.
No comments:
Post a Comment