Saturday, November 1, 2014

WAZIRI WA FEDHA WA MAREKANI AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATU MBALIMBALI DAR


Waziri wa fedha wa Marekani, Jacob J. Lew, akiwa katika picha ya pamoja na askari waliotekeleza ulinzi wakati wa ziara yake hapa nchini. Hapa ilikuwa muda mfupi baada ya kabla ya kuondoka jijini Jumanne jioni kwenye hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro Hotel, jijini Dar es Salaam.
Lew akiwa katika picha ya pamoja na madereva
Lew akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa ubalozi wa Marekani hapa nchini kutoka kitengo cha habari na mahusiano ya umma
Lew akiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP), Suleiman Kova, kwenye hoteli ya Hyatt Regency, saa chache kabla ya ,kuondoka jijini Dar esw Salaam, mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja iliyuojadili pamoja na mambo mengine, mahusiano ya kiuchumi baina ya Marekani na Tanzania pamoja na mradi wa Rais Barack Obama wa Power AfricaPicha kwa hiosani ya K-VIS

Jen.Traore ajitangaza rais Burkina Faso


Jenerali Honore Traore mkuu wa jeshi la Burkina Faso aliyejitangaza rais mpya wa nchi hiyo
Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore sasa amejitangaza kuwa rais baada ya aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kutangaza kujiuzulu.
Jenerali Traore ameshinikizwa na waandamanaji ambao walikuwa wanamtaka kuchukua usukani baada ya kuondoka kwa Bwana Compaore.
Bwana Compaore amesema kuwa amekubali kuondoka madarakani ili kutii matakwa ya waandamanaji ambao hawamtaki kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kutawala kwa miaka 27.
Bwana Compaore sasa ametaka uchaguzi mpya wa urais ufanyike baada ya siku 90.
Awali msemaji wa jeshi alikuwa amewaambia waandamanaji kuwa bwana Compaore hayuko tena madarakani huko Ouagadougou.
Maelfu ya waandamanji walikuwa wamerejea mabarabarani kwa siku ya pili
Hata hivyo hakubaini ikiwa afisa huyo wa kijeshi alikuwa akizungumza kwa niaba ya jeshi lote.
Jeshi lilisema kuwa litafanya mkutano na waandishi habari.
Siku ya Alhamisi waandamanaji waliokuwa wamekasirishwa na jitihada za rais za kuongeza muda wa uongozi wake baada ya kutawala kwa miaka 27 waliteketeza jengo la bunge na kuvamia kituo cha televisheni ya taifa.
Bwana Compaore alitupilia mbali jitihada za kubadilisha katiba ambayo ingemruhusu kuwania tena muhula mwingine kama rais lakini akasema kuwa angebaki madarakani kwa mwaka moja zaidi.
Chanzo bbc.

Boko Haram lawaoza wasichana wa Chibok



Wasichana wa Chibok waliodaiwa kuozwa na Boko Haram.kundi hilo limekana kuafikiana na serikali ya Nigeria
Kundi la wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria limekana madai kutoka kwa serikali ya Nigeria kuwa wameafikia makubaliano.
Akizungumza kwa njia ya kanda ya video, kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau alisema kuwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara kutoka eneo la Chibok kaskazini mwa Nigeria wamebadili dina na kuwa waislamu na kwamba wameolewa.
Abubakr Shekau
Shekau amasema kuwa hakujakuwa na majadiliano yoyote na serikali ya Nigeria.
Kiongozi huyo wa Boko Haram pia alitumia ujumbe huo kuthibitisha kuwa wanamshikilia raia mmoja mjerumani ambaye anakisiwa kuwa mwalimu aliyetekwa nyara mwezi Julai.
Serikali ya Nigeria inasema kuwa mazungumo na kundi Hilo yanaendelea kwenye nchi jirani ya Chad.