Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Seif Sharif Hamad (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya dola 4,000 za Marekani mshindi wa jumla wa Tuzo ya Uandishi Bora, mwandishi wa gazeti la The Citizen, Lucas Liganga, wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) Dar es Salaam, juzi usiku. Picha na Emmanuel Herman |
Sherehe za utoaji wa tuzo hizo ilifanyika jana
katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali
akiwamo Makamu wa Kwanza wa Rais, Seif Sharif Hamad ambaye alimwakilisha
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Mshindi wa jumla kwa mwaka 2012 ni Lucas Liganga
wa gazeti la The Citizen, ambaye ameifanya MCL kunyakua tuzo hiyo kwa
miaka miwili mfululizo ambapo mwaka 2011 tuzo hiyo ilichukuliwa na
Neville Meena wa gazeti la Mwananchi.
Washindi walipewa zawadi za magodoro, televisheni,
Ipad na vyeti, huku mshindi wa jumla akipewa dola 4,000 za kujiendeleza
kimasomo.
MCL iliingiza fainali waandishi 14 kati ya 66
walioteuliwa kuwania tuzo hizo ambao ni pamoja na Samweli Mwamkinga,
Florence Majani, Polycarp Machira, Tom Musoba, Elias Msuya, Leon Bahati,
Lucas Liganga, Shija Felician, Fredy Azzah, Joseph Zablon, Zephania
Ubwani, Tumaini Msowoya, Anthony Mayunga na Edward Qorro.
Mbali na kutoa mshindi wa jumla, waandishi sita wa
magazeti hayo walikuwa ndio wagombea pekee wa tuzo mbili za habari bora
ya Uchumi na Biashara na Majanga, huku Azzah akishinda tuzo ya habari
bora ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ambapo alikuwa peke yake na alichaguliwa
mara mbili kuwania tuzo hiyo.
Waandishi wa MCL walioshinda na tuzo zao katika
mabano ni Edward Qorro (Uchumi na Biashara), Lucas Liganga (Mazingira na
Malaria), Fredy Azzah (Ukimwi na Elimu), Anthony Mayunga (Utawala
Bora).
Wengine ni Florence Majani (Sayansi na Teknolojia
na Afya ya Uzazi), Samwel Mwakibinga (Mchora katuni bora), Zephania
Ubwani (Kilimo), Polycarp Machira (Majanga), Shija Felician (Tuzo ya
wazi).
Katika tuzo ya jumla MCL iliingiza waandishi watatu kati ya waandishi wanane waliochaguliwa kuwania tuzo hizo ambao ni Lucas Liganga, Fredy Azzah na Florence Majani.
Katika utoaji wa tuzo hizo, MCL ilifuatiwa na Shirika la Utangazaji (TBC) ambalo lilizoa tuzo nane, Afya Redio (6) na Kilimanjaro Film Institute (5).

Tuzo ya Uchumi na Biashara kwa upande wa
televisheni ilichukuliwa na John Lewanga wa TBC, tuzo ya michezo na
utamaduni kwa upande wa magazeti ilichukuliwa na Abdul Mohammed wa
gazeti la The African, Abdallah Majura wa ABM FM alishinda tuzo hiyo kwa
upande wa redio.
Tuzo ya mazingira upande wa redio ilichukuliwa na
Idd Juma Yusuf wa Afya Redio, tuzo ya afya upande wa magazeti
ilichukuliwa na Beatrice Shayo wa Nipashe na upande wa redio
ilichukuliwa na Gervas Hubile wa TBC-Taifa.
Tuzo za Ukimwi na VVU upande wa redio ilikwenda kwa Andrew Kiwanyi wa Kilimanjaro Film Institute.
Tuzo ya habari za watoto upande wa magazeti ilichukuliwa na Shadrack Sagati wa Habari Leo, upande wa Televisheni alichukua Daniel Kaminyoge wa Kilimanjaro Film Institute, upande wa redio ilichukuliwa na Mwamini Andrew wa TBC.
Utawala bora upande wa Televisheni ilichukuliwa na Jamal Hashim Said wa TBC, upande wa Redio ilichukuliwa na Noel Thompson wa Afya Redio.
Tuzo za habari za jinsia kwa upande wa magazeti ilichukuliwa na Husna Mohammed wa Zanzibar Leo, upande wa Televisheni tuzo hiyo ilichukuliwa na Bernard Mwaituka Televisheni Iringa.
Tuzo ya Sayansi na Teknolojia upande wa televisheni ilichukuliwa na Rose Kibaja wa TBC na upande wa redio ilichukuliwa na Abel Onesmo wa Clouds FM.

Upande wa tuzo za habari za Majanga kwa upande wa
redio alichukua Noel Thompson wa Afya Redio, habari za malaria kwa
upande wa Televisheni alichukua Dotto Mnyadi wa TBC na upande wa redio
ilichukuliwa na Faraja Sendegeya wa Afya Redio.
No comments:
Post a Comment