Friday, February 21, 2014

Muundo wa Muungano: Serikali Tatu, Moja, Mbili? Zote!-Zitto Kabwe


Mwalimu Azaveli Lwaitama ni mwalimu na mlezi wangu nje ya darasa. Alipokuwa Katibu wa Umoja wa Wanataaluma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mimi nilikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Idara ya Uchumi. Nilikuwa nashinda kwenye Ofisi ya UDASA tukijadiliana kuhusu Umajumui wa Afrika (Pan-Africanism), Ujamaa na harakati za kulinda haki za watu. Ilikuwa ni nadra kwa mwanafunzi wa uchumi kuwa karibu na mwalimu wa lugha na mnadharia mkubwa. Wanafunzi wa uchumi tulikuwa tunajidai na kujivuna. Tulikuwa tunajiona bora sana maana darasa letu halikuwa linazidi watu 40 na kwa kweli wote hawamalizi. Darasa langu tulimaliza wanafunzi 25 tu kati ya 40 tulioanza. Mwalimu Lwaitama ni mpenzi mkubwa wa Muungano kama nilivyo mimi. Tumeapa kuulinda kwa namna yeyote ile. Yeye alikuwa mhafidhina (conservative) sana akitaka Muungano wa muundo huu aliouacha Mwalimu Nyerere. Mimi nataka kuulinda kwa kuufanyia marekebisho makubwa sana ya kimuundo. Hatukuwa tunakubaliana.

Wiki iliyopita Mwalimu Lwaitama kaandika kuhusu muundo wa Muungano katika makala zake za kila wiki katika gazeti la kimombo la The Citizen. Amebadili msimamo. Ameona sasa muundo wa Muungano ulivyo sio endelevu. Ametoa mapendekezo niliyoyatoa siku za nyuma katika mazungumzo yetu ingawa yeye bado anayasema kwa shingo upande. Lwaitama sasa anataka Serikali mbili zilizonyumbuliwa. Anapendekeza Waziri Mkuu wa Muungano mwenye nguvu za za kitendaji. Nampongeza kwa kuboresha mawazo yake.

Hata hivyo bado Mwalimu wangu na Watanzania wengi wamejikita katika mjadala wa Serikali ngapi. Idadi ya Serikali inaonekana kama ndio dawa ya kero za Muungano. Ni kweli Wazanzibari wanataka uhuru zaidi na wengine hawataki kabisa Muungano. Unawalalia. Unawanyima uhuru wa kuamua baadhi ya mambo yao na japo halisemwi unawanyima wanasiasa wa Zanzibar mamlaka ya masuala mengine ambayo yangewafanya wajilimbikizie madaraka.

Huku bara napo kuna watu, tena wanaongezeka kwa kasi kweli kweli, wakitaka Tanganyika yao. Tena wengi vijana. Demografia zetu zinaonyesha kwamba Watanganyika waliozaliwa Tanganyika ni takribani asilimia 12 tu ya Watanzania. Asilimia 70 ya Watanzania wamezaliwa wakati Muungano umeshasherehekea miaka 15 ya kuzaliwa kwake. Lakini wanataka Tanganyika yao. Wamechoshwa na kelele za Wazanzibari. Hawawataki Wazanzibari kujaa kwenye Bunge la Muungano wakati wapo kiduchu sana. Wanasiasa nao, japo hawasemi waziwazi wanataka wawe na mamlaka zaidi bila kulazimika kushauriana na wanasiasa wa Zanzibar. Linapokuja suala la wagombea Urais ndio kabisa wanakereka kutafuta mgombea mwenza kutoka Zanzibar. Wachambuzi wa historia za kisiasa siku wakiamua kufanya tafiti watachoka na roho zao watakapoona aina za wagombea wenza ambao wagombea Urais huteua, hasa kutoka sisi vyama vya upinzani.

Kimsingi idadi ya wapinga Muungano inazidi kuongezeka siku hata siku. Ukiwauliza kwa nini hawataki Muungano wanasema aah, basi tu. Kama ni Mzanzibari atasema Tanganyika wanatutawala. Kama ni Mtanganyika atasema Wazanzibari wamezidi kelele, tunataka Tanganyika yetu. Sisi ‘Unionists’ (Wanamuungano) nao hatuna majibu ya kuridhisha sana na ya kukonga nyoyo. Isipokuwa tu, Muungano huu ni wa aina yake Afrika na Duniani. Ni alama pekee ya kuonyesha Mwafrika kupinga mipaka ya kikoloni. Sasa hili haliwaingii kichwani ‘secessionists’ (Wanautengano) na hatuna la kuwasaidia. Lakini ni lazima tuurekebishe Muungano huu. Ulivyo sasa utavunjika tu. Kuulinda Muungano ni kuufanyia marekebisho makubwa. Mwalimu Lwaitama kaliona hilo. Pendekezo lake liboreshwe sasa. Sio rahisi sana.

Sasa tufanyeje? Serikali moja itaimeza Zanzibar. Serikali Tatu ni gharama kuendesha na Serikali mbili zimeimeza Tanganyika na watu wanataka Tanganyika yao na zinainyima uhuru Zanzibar na watu wanataka wawe huru zaidi. Mfumo wa Serikali ngapi na kadhalika ni moja ya mikakati ya wanasiasa katika kusaka vyeo. Sisemi sio halali kujadili lakini kiukweli mfumo gani wa Muungano hautaongeza fungu la dagaa kwa mwananchi wa Kagongo au sinia la ubwabwa kwa mwananchi wa Mkanyageni. Waingereza wana msemo ‘unataka kula keki yako na kubaki nayo’, basi tuwe na Serikali zote.

Nimeanza na Mwalimu Azaveli Lwaitama. Naboresha hoja yake kwa kurudia niliyowahi kuyasema huko nyuma kuhusu muundo wa Muungano. Tuwe na Dola Moja tu. Ndio, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wala sio Shirikisho la Tanzania (kwanza litatuondoa kwenye kiti chetu kule Umoja wa Mataifa maana kwa jina letu sisi tunakaa katikati ya Uingereza na Marekani. Katikakati ya mabwana wakubwa, labda ndio maana wanatupa misaada sana, unajuaje?). Tuwe na Rais mmoja tu mwenye mamlaka kamili ya Asasi za Dola – Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Uhamiaji, Sera za Fedha na jukumu la jumla la kusimamia ustawi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Achaguliwe na Watanzania wote wa pande zote mbili za Muungano kwa kupata zaidi ya nusu ya kura za pande zote za Muungano. Tuachane na mambo ya Mgombea Mwenza. Tumejaribu tumeona hana maana zaidi ya kutembea na mikasi tu.

Zanzibar iwe na Waziri Mkuu Mtendaji kwa masuala yote ambayo sio ya Muungano. Tanganyika iwe na Waziri Mkuu Mtendaji kwa masuala yote ambayo sio ya Muungano. Hawa watateuliwa na Rais wa Muungano kutoka chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika na Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Wote watakuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa utaratibu kwamba iwapo Rais anatoka Zanzibar, basi Waziri Mkuu wa Tanganyika atakuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili wa Rais. Kule kule kwenye misingi haswa ya Muungano. Hawa wataongoza Mabaraza yao ya Mawaziri na watakuwa na nguvu ya kuteua na kufukuza Mawaziri wanavyotaka. Hawatakuwa Wabunge katika Bunge la Muungano.

Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye Wajumbe wasiozidi 101 pamoja na Rais wa Bunge la Muungano. Wabunge wa Muungano watatoka kwenye mikoa (au Majimbo kama sera ya Majimbo itakubalika). Kwa utaratibu wa sasa kila mkoa utachagua wabunge 2 mmoja mwanamke mmoja mwanaume kwenda Bunge la Muungano. Wajumbe wa Ziada watatokana na uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata kwenye kura za Rais wa Muungano. Idadi hii yaweza kupunguzwa na hata kuwa na Wabunge 51 tu akiwemo Rais wa Bunge la Muungano ambapo kwa mikoa ya sasa kila mkoa utachagua Mbunge 1 na wengine watokane na uwiano. Rais wa masuala ya Muungano atakuwa Mkuu wa Shughuli za Serikali katika Bunge la Muungano na Rais kwa mwaka mara moja atahutubia Baraza la Taifa (Wabunge wa Bunge la Muungano na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka kila upande wa Muungano). Wazungu wanaita hotuba hii ‘State of the Union’ (Hali ya Taifa) na wengine huita ‘Queen’s Speech’ (Hotuba ya Malkia).

Mkuu wa nchi mmoja, Dola moja ya Jamhuri ya Muungano. Serikali mbili na kila upande una Serikali yake yenye mamlaka kamili ya maisha ya watu wao ya kila siku. Haya matatu pamoja na Serikali ndogo ya Muungano. Lakini tutakuwa tumepata kila kitu labda. Wenye kutaka Uhuru mpaka Zanzibar watapata. Wenye kutaka Tanganyika watapata na wenye kutaka Muungano kama Dola yenye nguvu watapata.

http://udadisi.blogspot.com/2012/05/zitto-na-lwaitama-mwalimu-na-mwanafunzi.html?m=1

Wednesday, February 19, 2014

Matokeo haya ya udiwani, wapinzani wajitafakari

Uchaguzi wa madiwani uliofanyika hivi karibuni katika kata 27 nchini, umezua majonzi ndani ya vyama vya upinzani, na hasa Chadema baada ya kuambulia kata tatu.
Licha ya vyama vingine vya upinzani kikiwemo Chama cha Wananchi (CUF) kukosa kabisa hata kata moja, huku NCCR-Mageuzi kikifanikiwa kutetea kata yake moja mkoani Kigoma, Chadema kinaugulia zaidi kutokana na nguvu iliyotumika dhidi ya CCM.
Kwanza Chadema kilisimimamisha wagogombea katika kata 26 kikilinganishwa na CCM iliyosimamisha wagombea katika kata zote 27. Mgombea mmoja wa Chadema alijitoa dakika za mwisho mkoani Tanga.
Isitoshe, uchaguzi huo umekuja wakati Chadema ikiwa katika Pperesheni Pamoja Daima (OPD) ambapo viongozi wa Taifa wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu, Willibrod Slaa walishiriki.
Operesheni hiyo ilikuwa katika misafara ya helkopta tatu zikiwa zimesheheni makada wa chama hicho wakishambulia kwa zaidi ya mikutano 80 nzani ya wiki mbili.
Hata hivyo, operesheni hiyo ilionekana kufukiza ubani kutokana na mgogoro uliokuwa ndani ya chama hicho ambapo aliyekuwa Naibu Katibu wa chama hicho, Zitto Kabwe ambaye alivuliwa nyadhifa zake na kukimbia mahakamani kupinga hatua hiyo, huku wenzake aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti mkoani Arusha, Samson Mwigamba wakifukuzwa uanachama.
Mbali na mikutano hiyo iliyokusanya watu wengi, Chadema iligusia masuala ya kitaifa na baadaye kujikita kwenye kata zenye uchaguzi na kupiga kampeni kwa wagombea wao.
Baada ya uchaguzi huo kufanyika Februari 9, matokeo yalionyesha kuipa CCM ushindi mkubwa katika kata 23.
Chadema kimeambulia kata tatu ambazo ni Sombetini, Arusha na Njombe mjini zilizokuwa za CCM na kutetea yak wake ya Kiborloni, Moshi.
Chama hicho kimepoteza kata zake za Bunda na Kigoma zilizokwenda CCM.
Uchaguzi huo ndio ulikuwa kipimo cha kukubalika kwa chama hicho hasa baada ya kutoka kwenye mgogoro wa ndani na huenda mgogoro uliokuwapo umekitikisa, hasa kutokana na baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya nao kuonyesha kuunga mkono kambi ya Zitto.

Ofisa habari wa chama hicho chadema, Tumaini Makene anasema licha ya kushinda kata tatu kati ya 27 chama hicho kimetoa upinzani wa kweli kwa kusimamisha wagombea kata 26, zikiwamo ambazo hakikuwa na nguvu, lakini kikapata kura nyingi.
Anasema wanaolinganisha matokeo hayo ya udiwani na mikutano ya chama hicho ya OPD iliyofanyika hivi karibuni, wanatakiwa kuangalia kura ambazo wagombea wa chama hicho wamepata.
“Wanaosema hayo, wamepotoka na hizo ni propaganda nyepesi,” inasema sehemu ya taarifa ya Makene.
Anasema lengo la mikutano ya OPD ilikuwa ni kuzungumzia mchakato wa Katiba Mpya, uboreshaji daftari la wapigakura, kuzungumzia rasilimali za nchi na ugumu wa maisha unaosababishwa na sera mbovu za CCM.
“Operesheni Pamoja Daima imeibua mambo mengi; Katiba Mpya, rasilimali za nchi na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi na suala la daftari la wapigakura mpaka kufikia hatua na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza kulifanyia maboresho,” anasema.
Anasema maeneo ambayo mwaka 2010 hawakusimamisha mgombea udiwani wala mbunge, wamepata kura nyingi.
Chaguzi zilizopita
Tangu uliporudishwa mfumo wa vyama vingi, CCM bado imeonekana kuwa na nguvu hasa vijijini kutokana na muundo wake.
Licha ya kushinda katika chaguzi kuu, CCM imekuwa ikishinda vizuri katika chaguzi za Serikali za mitaa.
Kwa mfano katika uchaguzi wa mwaka 2009, CCM ilishinda viti vya wenyeviti wa vijiji na mitaa 264,344 sawa na asilimia 93.86, kikifuatiwa na CUF kilichopata viti 8,034 sawa na asilimia 2.85, wakati Chadema kilipata viti 6,480 sawa na asilimia 2.28.
Vyama vingine vilivyoshiriki ni pamoja na United Democratic (UDP) kilichopata viti 1,434 sawa na asilimia 0.51, NCCR-Mageuzi viti 614, asilimia 0.22, TLP 570, sawa (0.2 %), Chausta 158 (0.06), UPDP (25), PPT Maendeleo (12), NRA (4), DP (3), SAU (3) na UMD viti viwili.

TANZANIA RAHA KWELI KWELI Eti Nani wameiba Sh480 bilioni Hazina-Mwananchi?

Ugumu uliopo hapa ni kwamba haijulikani kama fedha hizo zilizopotea zilitokana na kodi za wananchi au wafadhili ambao walichangia Sh842 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13.

Tangu gazeti dada la The Citizen lichapishe mwishoni mwa wiki habari za upotevu wa Sh480 bilioni katika Wizara ya Fedha, Serikali imekaa kimya kama vile wizi huo ni tukio la kawaida, hivyo halihitaji maelezo ya kina wala ya haraka. Wananchi walitegemea kwamba Serikali ingetoa kauli haraka iwezekanavyo kuhusu mazingira ya upotevu huo na hatua inazochukua kuwawajibisha wahusika.

Tunasema kiasi hicho cha fedha zilizoibwa ni kikubwa kwa sababu ni zaidi ya bajeti ya mwaka kwa baadhi ya wizara, zikiwamo wizara kubwa kama ya Uchukuzi ambayo katika mwaka wa fedha wa 2013/14, kwa mfano ilitengewa Sh491 bilioni.

Tunaambiwa Sh480 bilioni zilizopotea katika Wizara ya Fedha zinaweza kujenga kilomita 375 za barabara kwa kiwango cha lami ikiwa ni urefu wa kutoka Dar es Salaam hadi Gairo, kilomita chache kutoka Dodoma. Tujiulize kiasi hicho cha fedha kingeweza kugharamia madawati, zahanati na madarasa mangapi kwa ajili ya wagonjwa na wanafunzi wetu.

Pamoja na ukimya wa Serikali kuhusu wizi huo, tumetiwa moyo na hatua ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), ambayo imemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kuchunguza upotevu huo wa kiasi hicho kikubwa cha fedha ambacho kilitumika pasipo maelezo katika kipindi cha miaka miwili ya fedha cha 2012/13 na 2013/14.

Wasiwasi wa kamati hiyo ni kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kuwapo kwa mtandao mkubwa wa wizi wa fedha za Serikali katika Wizara ya Fedha. Jambo hilo limethibitishwa na vitendo vya wizi wa kimtandao ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya watumishi wake wakishirikiana na baadhi ya watendaji wa Tamisemi.

Ugumu uliopo hapa ni kwamba haijulikani kama fedha hizo zilizopotea zilitokana na kodi za wananchi au wafadhili ambao walichangia Sh842 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/13. Ni sahihi kabisa kwa Kamati hiyo ya Bunge kushangazwa na kuendelea kuwapo kwa vitendo vya ufisadi serikalini, hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba ripoti za CAG kila mwaka zimekuwa zikifichua wizi wa mabilioni ya fedha katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Kujirudia kwa vitendo hivyo kila mwaka ni ishara kwamba Serikali haina dhamira ya kupambana na vitendo hivyo.

Mwenendo huo wa Serikali unashangaza, hasa kutokana na ukweli kwamba mwaka 2013/14 ilikuwa na nakisi ya Sh847 bilioni katika bajeti yake. Hivyo, utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo ingekwama kama siyo kukopa mabilioni ya fedha kutoka vyanzo vya nje na ndani ya nchi.

Matokeo yake ni kuzidi kuongeza mzigo wa Deni la Taifa ambalo limefikia Sh27 trilioni sasa, huku ikishindwa kukusanya kodi na kupanua wigo wa vyanzo vya kodi. Ndiyo maana iko hoi kifedha na karibu shughuli zake zote zimesimama, huku ikisuasua kulipa mishahara ya watumishi wake.

Pamoja na hali hiyo mbaya kifedha, bado vitendo vya wizi na ufisadi serikalini vinaendelea kama tunavyoshuhudia vikishamiri katika Wizara ya Fedha. Ni jukumu la Serikali kudhibiti ubadhirifu na ufisadi miongoni mwa watumishi wake, vinginevyo uchumi wetu utazidi kudidimia. Kwa kuanzia iwasake na kuwawajibisha wote walioiba Sh480 bilioni kutoka Hazina.

Tuesday, February 18, 2014

TAARIFA RASMI YA CCM

KAMATI YA MAADILI CCM

TAARIFA RASMI YA CCM
Kati ya tarehe 13/02/2014 na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama.

Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013.

Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:-

1. Ndgugu Frederick Sumaye
2. Ndugu Edward Lowasa
3. Ndugu Bernard Membe
4. Ndugu Stephen Wassira
5. Ndugu January Makamba
6. Ndugu William Ngeleja

Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza adhabu. Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika.

Kwa ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-

1. Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).

2. Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii. Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo.

Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi.

Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni:-

“Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.”

Kamati Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama.

Aidha, Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu za Chama.

Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI,
18/02/2014

Monday, February 17, 2014

Mh Rais, nakusalimu!-Lema Godbless


Kauli yako iliyonukuliwa na vyombo mbambali mbali vya habari wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wako wa NEC (CCM ) ni kauli hatari na yenye laana kubwa sana ya damu za Watu wengi katika Taifa letu. Ninaona wakati mgumu mwingine ambao Taifa letu linaingia kwa sababu ya kauli yako ambayo sasa imetangaza mauaji rasmi yatakayoongozwa na Viongozi mbali mbali wa CCM Nchi nzima huku Polisi wakiendelea kusimamia kama kawaida yao.

Mh Rais , Kwa mujibu wa maneno yako umethibitishia Umma wa Watanzania kuwa mmejadiliana kwenye kamati Kuu na kukubaliana kuwa sasa yale mambo mliyokuwa mnayafanya kwa kificho sasa yamethibitishwa na Kamati Kuu ya Chama chako na kutangazwa na wewe mwenyewe kuwa , kuumiza , kuua , kutesa na kudhalisha sasa imekuwa sera rasmi ya CCM na umeithibitisha kauli hiyo mbele ya Wajumbe wa Baraza Kuu la CCM ( NEC).

Mh Rais , kwa kauli hii naomba nikuambie kuwa umeamua kumalizia kipindi chako kwa mikono iliyojaa Damu na Roho za Watu . Nafasi uliyonayo ni kubwa sana sio jambo jepesi kuona makosa makubwa au madogo na kutubu , wapambe ni wengi ambao kwa kumsifu Mfalme hata kwa ujinga maisha yao na ya watoto wao yataendelea kuwa bora , lakini nakuhakikishia kwa kauli hii iko siku utajuta na kulaani ni kwanini ulitoa kauli mbaya na yenye hatia kama hii kwa Kiongozi mkubwa wa Nchi kama wewe . Vijana wa CCM sasa wamejipanga kuua na kuchinja hadharani kama ambavyo umeagiza wafanye na Polisi watakuwa Kimya kabisa kama ambavyo siku zote wamekuwa lakini mara hii watasaidia wazi wazi kabisa unyama wote utakaofanywa kwani wao pia wamesikia Amri yako na wewe ndio Mkuu wa Nchi hii.

Mh Rais, mambo mengi yanachangia kuvurugika kwa Amani lakini moja kubwa ni pale Polisi na Mahakama zitakaposhindwa kutenda wajibu wake katika kutenda haki haswa pale uonevu unapokuwa dhahiri . Naweza kutambua matendo yote mabaya yanayotokea wakati wa Uchaguzi kuwa yamesababishwa na Upendeleo wa Jeshi la Polisi kwa Wanachama wa CCM pindi wanapofanya uhalifu dhidi ya wenzao wa Vyama Vingine vya Siasa. Mwaka jana 2013 wakati wa uchaguzi wa marudio wa Madiwani wa kata nne Arusha Mjini watu zaidi ya 16 waliumizwa vibaya na Green Guard na matukio yote yaliripotiwa lakini mpaka leo hakuna Mtu aliyefikishwa mahakamani kujibu mashitaka, lakini unakumbuka na unajua kuwa mkutano wetu wa kufunga Kampeni hizo za Udiwani ulipigwa BOMU na Watu Wanne waliuuwa na Zaidi ya 100 kuumizwa vibaya na wengine wamebaki na Vilema hata leo na tumekuomba uunde tume ya Kimahakama ili tukuletee Wauaji wa watesaji wa tukio hilo lakini mpaka leo umegoma na badala yake zimekuwepo jitihada nyingi zinazofanywa na Jeshi la Polisi kubambikia Watu kesi nikiwemo mimi na kutesa watu kwa kiwango ambacho hakielezeki.

Mh Rais, Watu wameteswa na wanaendelea kuteswa sana katika Nchi hii na kazi hiyo inafanywa na Polisi na ccm na hapa ndipo mashaka katika jamii yanatokea na Jamii kuona ulinzi wao huko mikononi mwao na sio mikononi mwa Polisi na sheria za Nchi. Sasa umetangaza Watu wapigwe na wachinjwe hadharani , jambo ambalo nina uhakika nalo ni kwamba umeamua kuangamiza Nchi uliyoapa kuitetetea na ulioagiza wapigwe sina uhakika kama watakua wamelala chini wakati wanapigwa au wamefumba macho wakati wanateswa na kama itakuwa kinyume maana yake kutatokea Ugomvi ambao madhara yake mimi kwa sasa sielewi ila wewe MKUU uliyotoa amri utakuwa unajua.

Mh Rais, Wewe wewe ndiye Amiri Jeshi Mkuu umeshindwa kuamrisha Polisi walinde Raia na mali zao na sasa umeamua Watu wachinjane? kwa kauli hii unasubiri nini Ikulu ? Hata hivyo Nguvu ulizonazo sio Imara sana kama Nguvu alizonazo Mwenyezi Mungu . Mateso na Damu iliyomwagika katik

FDI stocks in Tanzania, top 10, 2011 in millions USD


South Africa 2,178
UK 1,344
Canada 1,080
Mauritius 650
Kenya 517
Swiss 276
Japan 197
Norway 183
Botswana 114
France 75

China not seen!

ANGALIA PICHA MSAFARA WA MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA KATIKA JIMBO LA KALENGA AZUIWA NA POLISI MKOANI IRINGA

Polisi mkoani Iringa wakiwa  wameuzua msafara  wa mgombea  ubunge jimbo la Kalenga,  Bi Grace Tendega kupitia Chadema kwa madai  hawakuwa na kibali cha kufanya  maandamano  hayo ya magari  hapa  ni eneo la lango la mji Samora ambapo msafara huo  ulikuwa ukitokea maeneo la Ndiuka kuelekea kwa msimamizi wa uchaguzi  ili kuchukua fomu.
Mgombea  ubunge wa  Chadema Kalenga, Grace Tendega baada ya  kuruhusiwa  gari lake kupita 


Hapa  polisi  wakimtazama  mgombea  huyo akipita  mbele yao
 Habari kamili  itakujia  hivi  punde  hapa  endeleo  kutembelea mtandao  huu 
PICHA NA FRANCIS GODWIN