Edward ngoyai lowasa na URAISI 2015-Fuatana na kamanda Jasiri Samweli Shami katibu Bavicha -Kahama
JE LOWASA NI MTU SAHIHI? Ni mzee nguli katika siasa za fitina Tanzania na afrika mashariki huku akisifika kwa maamuzi magumu anayoimba kila siku ilihali sijawahi kuona maamuzi aliyowahi kuyatoa ilhali amekalia ofisi za uma kwa zaidi ya nusu ya umri wake. Aidha nijaribu kuainisha baadhi ya matendo yake yenye utata ili watanzania wanaorubunika kirahisi wapate kuelewa aidha wakihamua wabaki na ushabiki ama wapone;- 1.Edward anatuhumiwa kwa kuchukua maji kwa ubavu kutoka Arumeru na kuyapeleka kusikojulikana [mito ya maji 3 kwa kuyafukia kwenye makalvat kina kirefu, pia yamewekewa patrol ya polisi ] ilihali akitoa tone na kuyaelekeza kwenye kambi ya jeshi monduli ili atumie fursa hiyo wanajeshi wayalinde kwamba ni yao kumbe ni kwa maslahi binafsi. Hapa tujiulize swali inakuweje jeshi linalotumia kodi za watanzania lilinde maji ya lowasa? Inakuweje askari polisi walinde maji kwa maslahi siyo ya kitaifa ama jamii bali ni uwekezaji wa lowasa? TAYARI TULIMUAGIZA JOSH. NASSARI MB. ALIFUATILIE LAKINI BADO HAJATOA JIBU. 2.RICHMOND – huu ulibainika ulikuwa mradi wake akishirikiana na swahiba wake kikwete ` `IF U HANDLE A TERRORIST U ARE A TERRORIST TOO `` NI KAULI YA WAMAREKANI. Tuhuma hii inamuangukia kutokana na kwamba ndiye aliyekuwa na dhamana ya shughuli za serikali na kushindwa kuwawajibisha wahusika aidha kwa kuwalinda wahuni hao pia naye uhuni unakuwa sehemu ya maisha yake ama ndiye mwenye mradi moja kwa moja maana hadi sasa RICHMOND ni sintofahamu. YOTE KWA YOTE ANAUTAKA URAISI WA TANZANIA ANAYOTUHUMIWA KUIFILISI. 3.UJANGILI –edward anahusishwa na vitendo vya ujangili mkoani arusha na manyara kupitia kivuli cha kampuni yake LEOPARD TOURS YENYE MAGARI YA CREAM Maana kuna LEOPARD TOURS yenye magari meupe inamilikiwa na tajiri wa kwanza nchini india mwenye hisa nyingi kwenye fast jet anaishi JIJINI HYDRA MT. MUMBAMBEY- india. Hii ni hatari kwa afya ya taifa letu endapo tutamkubali mtu hatari namna hii aitawale nchi yetu. NYERERE ALISEMA `EDD IKIWA NIMEKUPA WIZARA YA MIFUGO UMENIJENGEA MAGOROFA NA UKWASI HUU JE NIKIKUPA NCHI ITAKUWEJE? Watanzania wenzangu nachelea kusema ikiwa kafanya haya akiwa chini ya mtu je siku akiwa kileleni itakuweje? 4.GAMBA- Lowasa ,change na rostam waliitwa magamba / wezi wa rasilimali zetu siyo na shami bali na mkuu wan chi,tena walitajwa na pius msekwa na wakapewa siku tisini waachie ngazi jambo ambalo lisingetosha maana ikiwa jinai imefanyika muhamuzi ni mahakama, aghalabu hata hako kaadhabu ka ubabaishaji alikokabidhiwa nape kameishia mitini amemalizia kwa kusema `JK HATUKUKUTANA BARABARANI`` Hivyo ikadhihirisha kwamba madili wanapiga wote kwa yamini. Bado huyu mtu aliyetajwa kwamba ni mchafu leo hii anaitia watu nyama wanajisahau na kuanza kumuita jembe `POLE SANA MMA SHELUKINDO` KWA KUJITOA FAHAMU…….. KWA HIYO MNATAKA KUSEMA GAMBA/ MWIZI APEWE NCHI AIONGOZE? Watanzania mkiamua kufanya kinyesi kwamba ni chakula sawa lakini hata mungu ataumia sana endapo mtajaribu hili. 5.uadilifu, mzee huyu kwa orodha hii chache suala la uadilifu ni sifuri ,ikiwa anadiriki kutumia ofisi ya umma kwa maslahi binafsi kama anavyotumia jeshi na polisi huko arumeru. 6. NGURDOTO MOTEL -kuna sintofahamu kubwa juu ya umiliki wa hii hoteli yenye kubeba maraisi 30 ndani ya ikulu imara isiyoingiza bomu wala risasi ambapo nimeifuatilia kwa uendeshaji wake inadaiwa kukwepa mapato na shuru mbalimbali jambo ambalo lilikuwa kwenye ilani yangu wakati nilipokuwa natafuta kiti cha arumeru mashariki. Hili ni jambo hatari sana kwa ustawi wa taifa letu kwa kiongozi wa juu mwenye ushawishi kufanya jambo kama hili nab ado anahitaji uraisi. 7. PIA ANAHUSISHWA NA UMILIKI WA ANAPA [ MOMELA NATIONAL PARK ] inayomuingizia ukwasi bila kulipa kodi kinyume na katiba ya nchi. IKIWA MNAHISI NIMEMUONEA NIMETUMIA UHURU WANGU WA KUHOJI ,KUDADISI NA NI JUKUMU LA SERIKALI KUHAKIKISHA NAPATA HIZI TAARIFA KWA WAKATI NA SIYO KUNIPIGIA CM ZA VITISHO.LIWALO NA LIWE LAKINI HAKI YA WATANZANIA ISIPOTEE. `` KATIKA SUALA LA UKOMBOZI NI LAZIMA WENGINE WAKUBALI KUWA MBEGU`` WENU KAMANDA JASIRI SAMWEL SHAMI KATIBU BAVICHA – KAHAMA.
No comments:
Post a Comment