Thursday, November 8, 2012

Rais wa Syria Bashar Al Asaad amesema kamwe hataondoka nchini humo na badala yake atafia nchini Syria.

Rais Bashar ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha television cha Urusi cha Russia Today news kwamba ataishi na kufia nchini humo.
Rais Bashar amesema hatarajii nchi za Magharibi zitaivamia kijeshi Syria na kuonya kama watachukua hatua hiyo itasababisha madhara makubwa duniani kote.
Mkuu wa kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu amesema hali ya kibinaadamau nchini Syria kwa sasa ni mbaya mno kiasi cha kuwa wanang'ang'ana kukabiliana nayo.
Peter Maurer amesema ICRC haiwezi kufika katika maeneo yote ya nchi hiyo.Katika mji mkuu Damascus, mapigano yamekithiri wakati wanamgambo na vikosi vya usalama vimekabiliana katika baadhi ya wilaya.
Katika mji mkuu wa Qatar Doha, kundi kuu la upinzani, baraza la kitaiaf la Syria, limewachagua wanachama 40 katika afisi kuu ya baraza hilo na lina uwakilishi mkubwa wa dini ya kiislamu.
Hakuna wanawake waliochaguliwa Wamesema rais atachaguliwa siku ya Ijumaa.

No comments:

Post a Comment