Monday, November 12, 2012

Mafataki ya gharama ya Romney yadoda


MGOMBEA wa Urais wa Marekani aliyeshindwa katika uchaguzi uliofanyika Jumanne wiki hii, Mitt Romney ameelezewa kuathiriwa na matokeo hayo, kwa kuwa alitarajia ushindi kutokana na mtizamo aliokuwa akipewa na washauri wake.

Taarifa za baada ya uchaguzi huo zilieleza jana kwamba hadi hatua ya mwisho wakati wapiga kura wakielekea vituoni, tayari Romney alishajiandaa kusherehekea ushindi ikiwemo kununua mafataki maalum yenye thamani ya zaidi ya Dola 25,000 na vifaa vingine.

“Lakini mabo hatakwenda kama Romney alivyotarajia, hasa baada ya matokeo kutangazwa siku ya uchaguzi,” alieleza mmoja wa wafuatiliaji wa karibu wa harakati za Romney kutoka kituo cha Boston Globe, Glen Johnson.

“Wafuasi wa Republican walishajiandaa kusherehekea kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa 45 wa Marekani, hasa kwa kujaribu kuangalia historia, huku wakiwa wameandaa mafataki ya gharama kubwa ambaye yalitakiwa kuwashwa kwa dakika nane katika makao makuu ya chama chake huko Boston,” alieleza.

Hata hivyo, baada ya kutangazwa matokeo, hatua ya Romney kuamua kumpigia Obama simu kukubali kushindwa, mkewe, Ann Romnei alijikuta akidondosha machozi, huku aliyekuwa mgombea mwenza, Paul Ryan akionekana kupatwa na mshtuko na mkewe pia akijikuta akidondosha machozi.

Kikosi cha kampeni cha Romney kilidaiwa kununua mafataki hayo ya kifahari yenye rangi nyekundu, nyeupa na bluu kama moja ya zana za kuonyesha uzalendo na ushindi kwa mgombea wao.

Wachambuzi kutoka gazeti la Wall Street Journal, Sara Murray and Patrick O'Connor walisema kwamba mshtuko mkubwa alioupata Romney ulitokana na ukweli kwamba alitumia kiasi kikubwa cha fedha katika kampeni hizo, lakini aliamua kukubali matokeo katika hatua za awali.

“Romney alitumia kiasi kikubwa sana cha fedha ili kuteuliwa na chama chake kuwania nafasi hiyo. Pia alitumia wiki na miezi ya awali ya kampeni zake kuchangisha fedha huko California, Texas, na New York, maeneo ambao hayakuwa mazuri kwake kisiasa,” walieleza.

Romney aliweza kuchagisa zaidi ya Dola800 milioni lakini kwa gharama kubwa kisiasa kwake pia, hasa kwa kujikuta akimpa nafasi nzuri Obama kumchambua na kumharibia taswira yake katika kampeni zake.

Hata baada ya kumalizika kwa uchaguzi, tahmini imekuwa ikiendelea kufanyika kuhusu kile kilichokuwa kikitokea nyuma ya pazia na mambo mengi sasa yamekuwa yakiwekwa wazi.

Washirika wa Romney tangu awali walitarajia kuwa matokeo ya kura yatamshusha Obama has akutokana na walivyokuwa wakifanya tathmini ya mwenendo wa kampeni na midahalo, lakini hata hivyo, katika matokeo ya mwisho Obama alifanikiwa kutetea kiti chake cha urais.

No comments:

Post a Comment