Katika kile kinachodaiwa kuwa ni kuhujuma dhidi ya
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, baadhi ya vipeperushi
vimeonekana katika maeneo mbalimbali mjini hapa vikiwa na ujumbe
unaosomeka: “CCM inayumba kwa pamoja tumpunguzie mzigo mheshimiwa Rais
kwa kumvua kofia moja ya uenyekiti, nina imani kwa pamoja tutashinda,
piga kura ya hapana kwake, CCM oyeeee.”
Vipeperushi hivyo vimetawanywa mitaani na watu wasiojulikana tangu juzi.
Habari
zaidi zinaeleza kuwa moja ya kundi ndani ya chama hicho, ndilo
linalohusishwa na mkakati huo likidaiwa kwamba linataka Makamu
Mwenyekiti wa Zanzibar, Amani Karume apewe nafasi hiyo ili Rais Kikwete
abaki na madaraka ya urais pekee.
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo,
Agustino Matefu kutoka mkoani Morogoro alisema wamefuatilia na kubaini
kuwa kuna makada wazito ndani ya chama hicho wanaohusika... “Hiki hapa
kipeperushi mnaweza kukiona wenyewe,” alisema huku akionyesha.
Alisema
mpango huo unasukwa na kundi ambalo linaongoza kwa kutoa rushwa katika
chaguzi za chama hicho na kuandaa mtandao wa viongozi mbalimbali kwa
lengo la kuwasaidia katika kampeni za urais.
Mjumbe huyo aliyekwenda
mbali zaidi na kueleza kuwa Mtandao huo umetenga kiasi cha Sh5 bilioni
kuwasaidia wagombea wao 10 katika nafasi za ujumbe wa Nec na kudai
kwamba orodha ya wajumbe wao imekuwa ikipitishwa kwa wapiga kura
kuwashawishi wawapigie kura nyingi.
Akizungumzia madai hayo,
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa alisema hajaviona
vipeperushi hivyo, lakini akasema kitendo hicho kimefanywa na watu
wapuuzi ambao hawaijui CCM.
Alisema kitendo hicho hakijafanywa na wanaCCM wa Dodoma na kwamba watafanya kila linalowezekana kuwabaini watu hao.
Wakati
wajumbe hao wakichuana kuwania nafasi hiyo kupitia kapu, uchaguzi wa
Mjumbe wa Nec wilayani Longido, Arusha umebaki kitendawili.
Uchaguzi
huo ulikwama mwezi uliopita baada ya wagombea kushindwa kufikisha nusu
ya kura. Hao walikuwa Mbunge wa Loliondo, Lekule Laiser aliyepata kura
417, Peter Lemshau (381) na mwingine aliyeambulia kura 58.
Habari
zilizopatikana jana zinasema mmoja wa wagombea yupo Dodoma kukutana na
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama kujua hatima ya uchaguzi huo.
Chanzo-Mwananchi
No comments:
Post a Comment