Lord Eyez wa N2N Soldiers
amefanya Exclusive interview na millardayo.com na kuzungumza ishu kadhaa
kuhusu tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la Ommy Dimpoz.
Kwanza alianza kwa
kuzungumza na wale mashabiki zake waliotoa vitisho vya kumdhuru Ommy
Dimpoz huku wengine wakimwambia asikanyage Arusha na hiyo yote ni
kutokana na kukasirishwa na kitendo cha Ommy Dimpoz kusambaza picha za
Lord Eyez na kumuita mwizi.
Namkariri Eyez akisema “mi
ninachosema wasimuhukumu mtu kwanza wala wasipandwe, wanahitaji kujua
ukweli na wasifanye matukio yoyote ambayo ni ya uvunjaji wa sheria na
pia wachague marafiki, wawe wastaarabu, wawe wapole na wawe na subira…
wasimjengee chuki binadamu, mi mwenyewe nimekua mtu wa kusamehe sana
ndio maana nakwambia wamwachie Mungu, kwa kuwa mimi sina chuki na mtu
siwezi kumshauri mtu awe na chuki na mtu lakini malipo ni hapahapa
duniani na Mungu yupo wamwamini sana sababu ndio anafanya kila kitu”
Jinsi alivyokamatwa siku
ya tukio, Lord Eyez amesema alipigiwa simu na mwanaume alafu baadae
akaongea na mwanamke ambae alitaka waonane Kinondoni mida hiyo ambapo
alikwenda kwenye eneo la tukio bila kujua kitatokea nini.
Alipofika zilikuja gari 3
zenye watu wengi ikabidi ahamaki, wakaanza kama kumzingua na jamaa mmoja
akasikika akisema huyu atatusaidia kumpata tunaemtafuta, walimshikilia
Lord Eyez kwa masaa yasiyopungua manne kwa mujibu wa maelezo ya Wakili
wake.
Wakati wamemshikilia Lord
Eyez akasema huyo jamaa wanaedhani ni mshkaji wake ambae ndio anadaiwa
kuhusika na wizi wamejuana hazipiti hata wiki mbili na hamjui kihivyo,
baada ya hapo walimchukua mpaka kwenye eneo lilipo gari la Ommy Dimpoz
lililoibiwa vifaa ambapo Eyez anasema walipofika kwenye hilo gari, kweli
alishuka ili aliangalie kwa sababu alikua anashangaa pia lakini
akapigwa picha ambazo baadae ndio zilisambazwa kwamba ni ushahidi wa
wizi aliofanya.
Eyez amesema watu hao
waliomshikilia kwa saa kadhaa walitaka kumzingua na kumpiga lakini
kiongozi wao alizuia mtu asimguse.
Amesema hii ni mara yake
ya kwanza kushikiliwa na polisi ambapo hii ya juzi alishikiliwa kwa
zaidi ya siku kumi na mbili na anasisitiza kwamba sio kweli yeye ni
mwizi, hawezi kuifanyia jamii mambo kama hayo.
Kuna mengine aliyoyaongea
Lord Eyez ambayo ni Exclusive on millardayo.com na AMPLIFAYA ya CLOUDS
FM, utaendelea kuyasoma na kuyasikia siku baada ya siku.
facebook.com/millardayo
twitter.com/millardayo
No comments:
Post a Comment