Monday, November 12, 2012

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu BBC kulipwa,ni aliyejiuzulu

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa BBC, George Entwistle, atapewa mshahara wa mwaka mzima - kiasi cha zaidi ya dola 715,000 - baada ya kujiuzulu.
Bwana Entwistle alijiuzulu baada ya kipindi cha televisheni nchini Uingereza cha Newsnight kutoa habari potofu kwamba mwanasiasa mmoja wa zamani Muingereza aliwadhulumu watoto kijinsia.
Msemaji wa BBC Trust alisema Bwana Entwistle atapewa mshahara huo kwa sababu ataendelea kuisaidia BBC katika shuguli kadhaa, zikiwepo tume mbili za uchunguzi zinazoendela.
Hata hivyo, katibu wa kamati moja ya bunge alihoji mshahara huo kwa sababu Bwanda Entwistle amekuwa mkurugenzi kwa muda wa siku 54 tu.

No comments:

Post a Comment